Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi
funguo za Trekta kwa Mwenyekiti kwa vijana Tumsume Shemgogo lililotolewa
na chama cha Mapunduzi CCM kwa vijana wa mkoa wa Njombe katika
makabidhiano yaloyofanyika kwenye Kambi ya vijana iliyopo kwenye kijiji
cha Mlengu Kata ya Kiangala Tarafa ya Ikuo mkoani Njombe ambapo kambi
hiyo ina eneo lenye ukubwa wa hekta 300 za mashamba, Kinana aliahidi
kutoa trekta hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Njombe mwezi
Agosti mwaka huu baada ya kuelezwa jinsi vijana hao walivyojiunga
pamoja katika kikundi na kuamua kushughulika na kilimo ili kujkwamua
kiuchumi, Leo Abdulrahman Kinana alishiriki kulima kwa trekta kabla ya
kukabidhi trekta hilo kama anavyoonekana katika baadhi ya picha akilima
shambani kwa trekta. Kushoto anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Katika Ziara hiyo
Kinana pia ameongozana na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kamataifa na Mbunge wa kuteuliwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-MAKETE-NJOMBE) Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilima shambani kabla ya kukabidhi trekta hilo. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiliendesha kwa umakini kabisa. Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kamataifa na Mbunge
wa kuteuliwa akikumbatiana kwa furaha na Mkuu wa Wilaya ya Makete
Josephin Matiro mara baada ya kuwasili katika eneo la mapokezi huko
Chimala Mbeya. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia
akizungumza na Kapten mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kuagana na Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa pili kutoka kushoto na viongozi
wengine wakati alipowasili katika eneo la Mapokezi huko Chimala mkoani
Mbeya leo Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndg, Deo Sanga “Jah People” akizungumza wakati wa mapokezi hayo kulia ni Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kutoka
kushoto ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kucheza ngoma ya kabila la Wawanji huko linalopatikana mkoani Njombe. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
vijana wa Kambi ya Mlengu kabla ya kukabidhi trekta kwa vijana hao. Wananchi wa kijiji cha Mlengu wakimsikiliza Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungmza nao. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia
jambo wakati alipokagua darasa la ushonaji wa nguo katika chuo cha Veta
mjini Makete Kushoto ni Dr. Asha Rose Migiro na katikati ni Mkurugenzi
wa Veta Kanda ya Kusini Monica Mbele, Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na
Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kusini Monica Mbele wakati alipokagua chua
cha Veta mjini Makete leo kushoto ni Josephin Matiro Mkuu wa Wilaya ya
Makete. Injini Asifiwe Swalo mwalimu wa chuo cha VETA Makete akitoa maelezo kwa Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati
alipotembelea chuoni hapo na kukagua shughuli mbalimbali zinazoendeshwa
na chuo hicho, kulia ni Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kusini Monica Mbele. Mwanafuzni wa fani ya ujenzi Abel Mbilinyi akimuelezea Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi
wanavyofyatua matofari yaliyochanaganywa udongo wa kawaida na saruji
kidogo na faida zake Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapten Aseri Msangi akiuliza swali kwa mwanafunzi Tito Fungo uimara wa matofari hayo huku Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Dr. Asha Rose Migiro wakisikiliza kwa makini. Nape Nnauye akijenga njia zinazopita chuni hapo kwa matofari madogo huku Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakiangalia. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu chuoni hapo. Dr.
Asha Rose Migiro katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa
wilaya ya Makete Josephin Matiro kushoto na Monica Mbele Mkurugenzi wa
VETA kanda ya Kusini. Picha ya pamoja ikipigwa
Comments
Post a Comment