

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (Chadema), marehemu Chacha Zakayo Wangwe enzi za uhai wake.
Hussein Ramadhan Shekilango; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe (CCM)
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (utawala). Alifariki dunia Mei
11, 1980 kwa ajali ya ndege iliyotokea kwenye milima ya Arusha.
Kumuenzi, serikali iliipa jina Barabara ya Shekilango iliyopo Sinza,
Dar.
Juma Jamaldin Akukweti; alikuwa Mbunge wa
Jimbo la Tunduru (CCM) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).
Alifariki Januari 4, 2007 Hospitali ya Johannesburg, siku chache baada
ya ajali ya ndege iliyoanguka ikitaka kupaa Desemba 16, 2006 jijini
Mbeya alikokuwa kwa shughuli za kikazi.

Salome Joseph Mbatia; alikuwa Mbunge wa
Viti Maalum-CCM na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.
Alifariki papo hapo Oktoba 23, 2010 katika ajali mbaya ya gari lake aina
ya Nissan Patrol kugongana uso kwa uso na Fusso maeneo ya Kibena, akiwa
njiani kwenda Njombe.

Mussa Khamis Silima; alikuwa Mbunge wa
Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini, Zanzibar. Alifariki katika ajali
ya gari Agosti 23, 2011 maeneo ya Nzuguni, Dodoma pamoja na mkewe,
Mwanaheri Fahari. Marehemu alikuwa akielekea bungeni Dodoma kutokea Dar.
Edward Moringe Sokoine; alikuwa Mbunge wa Jimbo laMonduli (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania. Alifariki kwa ajali Aprili 12, 1984 eneo la Dumila, Morogoro. Ili kumuenzi, serikali imetoa jina la Barabara ya Sokoine, ipo Posta jijini Dar na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro.
Comments
Post a Comment