Skip to main content

WOLPER AMSALITI KAJALA KWA WEMA

Na Musa mateja
UNAFIKI 100%! Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ‘Kay’, ameibua mshangao baada ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa haziivi na Kay.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper akishoo love na Wema Sepetu.
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI
Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar.
WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa ‘wamemisiana’.
Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa wakinong’onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minong’ono ikaanza.
WATAALAM WA UBUYU
Kitendo cha Wema kutumia dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper, kilitafsiriwa na wataalam au wafuatiliaji wa mambo ya watu (ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema.
Wema Sepetu akimhagi Jacqueline Wolper.
“Mh! Mwenzangu makubwa, huyu Wolper si ni Timu Kajala? Inakuwaje anatoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa adui wa Kajala? Hapa kuna tatizo, unafiki kwa mastaa kamwe hauwezi kuisha,” alisikika mtoa ubuyu mmoja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.
AKUMBUSHA VITA YAO
Kama hiyo haitoshi, mtoa ubuyu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema, ukiachilia mbali Wolper kuwa karibu na Kajala lakini hata yeye (Wolper) alikuwa kwenye vita nzito na Wema kwa kudaiwa ‘kushea’ naye penzi la msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Wolper jamani mnafiki...si ndiyo huyuhuyu aliwahi kuingia kwenye vita nzito na Wema baada ya kudaiwa kuwa anadondoka dhambini na kipenzi cha Madam, Diamond? Yaani huu ni unafiki asilimia mia,” alisema mtoa ubuyu huyo.
TIMU KAJALA WAJA JUU
Baada ya Timu Kajala kusikia kwamba Wolper ‘ali-spendi’ vya kutosha na Madam kwenye bethidei hiyo, walikuja juu kisha wakamtolea uvivu na kuanza kumshambulia katika mitandao ya kijamii na kudai hafai kuwa timu yao.
Huku wakati huo huo... Jacqueline Wolper akishea urojo sahani moja na Kajala Masanja ‘Kay’.
“Wolper msaliti, ataendaje kwenye sherehe ya mpinzani wetu? Tena kama hiyo haitoshi, yeye anakumbatiana na Madam ambaye kwetu sisi hatusaidii lolote,” alisema mmoja wa Timu Kajala.
KUMBUKUMBU IPOJE?
Kabla ya siku hiyo, Wolper na Wema hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na kila sehemu ambayo utakumta Wolper, kamwe huwezi kuona Wema ametia maguu.
WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya paparazi wetu kushuhudia kitendo hicho ukumbini, alimfuata Wolper na kumuuliza ni kitu gani kilichowasababisha wapatane na kuoneshana ‘mahaba niue’ wakati nyuma ya pazia wana bifu? Msikie alichojibu:
“Ujue watu wengi sana wamekuwa wakidhani mimi na Wema tuna bifu, sijui kwa kuwa mimi nina ukaribu na Kajala au kwa kuwa hatujawahi kuwa pamoja, lakini ukweli mimi na Wema siyo waongeaji sana japokuwa huwa nikiweka picha au chochote kwenye Instagram, Wema huwa ana-like na mimi huwa na-like vitu vyake hivyo sidhani kama nilikuwa na tatizo naye sana,” alisema Wolper.



TUJIKUMBUSHE
Urafiki wa mastaa huwa mara nyingi haudumu, Wema ambaye hivi sasa shosti wake mkubwa ni Aunty, kabla aliwahi kuwa na urafiki na Snura Mushi, Jamilah wa Temba, Kajala na wote hao akawamwaga.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below: