Ni Ijumaa nyingine nzuri ninapokukaribisha msomaji wangu katika zulia jekundu la uwanja wetu huu ambao ni maalum kwa mambo yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Mada ambayo ningependa kujadiliana nawe msomaji wangu ni kama inavyojieleza kwenye kichwa cha habari.
Yawezekana wewe ni mwanaume au mwanamke ambaye unafanya kazi na umpendaye, awe ni mke, mchumba au mpenzi. Je, kuna faida gani unazozipata kutokana na kufanya kazi ofisi moja na umpendaye? Vipi kuhusu hasara na changamoto?
Bila kujali kama mmekutana sehemu ya kazi na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi au mlianza kabla lakini baadaye mkajikuta mkifanya kazi sehemu moja, lazima ujue kwamba zipo faida lakini kama hiyo haitoshi, zipo changamoto nyingi ambazo ni lazima ujue namna ya kuzishughulikia ili kuwa na uhusiano bora wa kimapenzi na amani ya nafsi yako.
FAIDA KUBWA
Faida kubwa ya kufanya kazi pamoja ni kwamba unapata muda wa kutosha wa kuwa karibu na mwenzi wako. Kwa wale ambao wana hulka ya wivu au wanashindwa kuwaamini wenzi wao, kufanya kazi pamoja huwasaidia kutulia kwa sababu watakuwa na uhakika na mahali walipo au shughuli wanayoifanya wenzi wao kwa sababu wanawaona na wanashinda nao siku nzima.

CHANGAMOTO ZAKE
Changamoto za kufanya kazi ofisi moja na umpendaye, huwa ni nyingi kuliko faida na usipokuwa makini zinaweza kusababisha kuyumba, kulegalega au kuvunjika kabisa kwa uhusiano wako wa kimapenzi na umpendaye.

Changamoto ya kwanza na kubwa huwa ni kushindwa kutenganisha mambo ya nyumbani na mambo ya kazini. Kama jana usiku mlikorofishana na mwenzi wako, uwezekano mkubwa ni kwamba chuki za nyumbani utazileta kazini na matokeo yake, ufanisi wa kazi utapungua.
Pia, kihulka binadamu ameumbwa kuwa na muda wa kukutana na watu wengine, kubadilishana mawazo na kuingiza vitu vipya kichwani. Sasa inapotokea wewe na mwenzi wako mnafanya kazi pamoja, ni kwamba mtajikuta muda mwingi mkiutumia pamoja na kushindwa kuchanganyika na watu wengine, jambo ambalo kitaalamu husababisha msongo wa mawazo.
Changamoto nyingine, ni pale inapotokea mmoja kati yenu ameharibu kazi. Kwa kawaida, mabosi huwa wakali inapotokea mfanyakazi amefanya kosa lililosababisha hasara, iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi.
Mabosi wengine hufikia hatua ya kuwafokea au kuwaadhibu waliofanya uzembe huo. Utajisikiaje mwenzi wako anapoadhibiwa mbele yako kwa sababu amefanya makosa kazini?
Vipi kuhusu mwenzi wako anapokorofishana na wafanyakazi wenzake? Wahenga walisema vikombe vinapokaa kabatini pamoja, havitakosa kugongana. Hivyo mwenzi wako anapofanya kazi, ni lazima itatokea akakorofishana na wafanyakazi wenzake.
Je, utajisikiaje kusikia mwenzi wako akitukanana au kupandishiana na mtu mwingine kwa sababu ya kazi? Kimsingi utaambulia ‘stress’ za kutosha ambazo huenda zikapunguza ufanisi wako wa kazi.
NINI CHA KUFANYA?
Licha ya changamoto nilizozieleza hapo juu, wapo wapendanao wengi ambao huweza kudumu na kuishi maisha ya furaha japokuwa wanafanya kazi ofisi moja. Hata wewe unaweza kuwa na uhusiano bora licha ya kuwa unafanya kazi ofisi moja na mwenzi wako endapo utazingatia mambo ya msingi ambayo nitakufafanulia kwa kina kwenye sehemu ya pili ya makala haya.

Usikose wiki ijayo ambapo tutaangalia kwa kina mbinu za kupambana na matatizo yanayotokea kazini kwa sababu ya kufanya kazi ofisi moja na mwenzi wako.
Comments
Post a Comment