ARUSHA
NA MWANDISHI WETU; AMANI JAMES
Uongozi wa mtaa wa
nanja kata ya moshono umekanusha kuwa sio wananchi wa mtaa huo ndio wanahusika
na utupaji tataka ovyo ndani ya mtaa huo, na kusema ni watu kutoka nje ya mtaa
huo ndio huleta taka hizo majira ya usiku na kuzitupa.
Hivyo mwenyekiti wa
mtaa huo Lilian Mmasi amesema kuwa tayari ameshaweka walinzi kwaajili ya
kuwakamata watu wanao tupa taka ndani ya
mta wake, na atakayekamatwa atalipa faini ya shilingi elfu hamsini (50000) na
atawajibilka kufanya usafi ndani ya mtaa
hiyo.
Sambamba na hilo
amesema kuwa walishapitisha sheria ya kila nyumba ndani ya mtaa wake kutoa
shilingi elfu moja kwa kila mwezi kwa lengo la kusaidia usafi ndani ya mtaa
huo, lakini hadi sasa mwitikio ya watu kutoa mchango huo ni mdogo.
Hata hivyo ameendelea
kusema kuwa kwa sasa kila mwananchi ni
lazima alipe mchango huo na asipolipa atapelekwa mahakamani na kushitakiwa kwa
kosa la kukataa kushiriki usafi ndani ya mtaa huo.
Mbali na hayo pia mwenyekiti huyo amekiri kuwa vitendo vya
ualifu umeongezeka mtaani hapo, lakini amewatoa hofu wananchi wake kwa kusema
kuwa kwa sasa kunautaratibu wanaouandaa ambao utakomesha tatizo la ualifu ndani
ya mtaa wake.
Comments
Post a Comment