Na Daudi Julian, Morogoro
MAPAMBANO zaidi ya sita ya ngumi za kulipwa yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, wiki hii, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, katika Manispaa ya Morogoro.
MAPAMBANO zaidi ya sita ya ngumi za kulipwa yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, wiki hii, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, katika Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza
na mtandao huu, msemaji wa mapambano hayo ambayo awali yalipangwa
kufanyika Novemba 24 kabla ya kurudishwa nyuma, Mohamed Jeilan alisema
maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba mabondia wote watakaopanda
ulingoni wapo katika mazoezi makali.
Jeilan
alisema lengo la mapambano hayo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa mjini
Morogoro, ni kuibua vipaji vya mabondia chipukizi na kuendeleza mchezo
huo kiujumla.
Alisema
mbali ya mabondia wa Morogoro, mabondia wachache kutoka jijini Dar es
Salaam pia wanatarajiwa kualikwa kwa lengo la kutoa changamoto katika
mapambano hayo.
“Kimsingi
maandalizi yanakwenda vizuri na mabondia wote hivi sasa wanaendelea
kujinoa chini ya makocha wao ili kuhakikisha wanafanya vizuri siku
hiyo”, alisema.
Msemaji
huyo amewataja baadhi ya mabondia watakaopanda ulingoni siku hiyo kuwa
ni George Masawe ‘G Mawe’, Athuman Dame, Miraji Abdallah ‘Kinditi One
Power’, Salum Saleh ‘Sure Boy’, Beta Kingalu na Ngoda Stopa.
Jeilan
ametoa wito kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi mkoani hapa kujitokeza kwa
wingi siku hiyo ya Ijumaa katika ukumbi huo ili kushuhudia mapambano
hayo.
“Mapambano
yatakuwa makali sana na yenye upinzani wa hali ya juu hivyo napenda
kutoa wito kwa mashabiki wa ngumi kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia
jinsi gani ngumi zinavyopigwa”, alisema
Comments
Post a Comment