Anayedaiwa kuwa mpenzi wa marehemu, Christina.
Mauaji hayo yalitokea juzi nje ya nyumba ya wanafamilia waliokumbwa na dhahama hiyo iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Katika mauaji hayo, Gabriel alidaiwa kumuua kwa risasi shemejiye
aliyejulikana kwa jina la Alfa Nando, kumjeruhi mchumba wake, Christina
Nando, mama mkwe wake (mama wa Christina), dereva wa familia aitwaye
Francis kisha kujimaliza mwenyewe.Mauaji hayo yalitokea juzi nje ya nyumba ya wanafamilia waliokumbwa na dhahama hiyo iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu rafiki mmoja wa marehemu Gabriel (jina lipo) alisema marehemu ambaye alikuwa mfanyabiashara wa magari jijini Mwanza aliaga kwenda Dar kumchunguza mchumba wake (Christina) kwa sababu alidokezwa kuwa shemeji yao huyo anamsaliti kwa kutembea na RPC ambaye jina lake halikupatikana.
Alidai kuwa, baada ya kufika Dar marehemu alimpigia simu na kumwambia kuwa, habari za Christina kutembea na RPC huyo ni za kweli na kwamba amepata habari anataka kusafiri hivyo hatakubali aende hiyo safari bila kumfanyia kitu kibaya.
Comments
Post a Comment