Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa tatu kutoka
kulia), akiongea na fundi ambaye anafanya shughuli za ujenzi katika
Daraja la Reli la Bahi-Kintinku. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara
kwenye daraja hilo na kupata taaarifa kuwa limekamilika kwa asilimia
98. Aidha daraja hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5. Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka
mbele), akishuka chini ya daraja la bahi-kintinku kuangalia maendeleo ya
ujenzi wake. Daraja hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC). Kukamilika kwa daraja hilo kutasababisha Treni za abiria na mizigo kupita kwa uhakika majira yote ya mwaka. Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi wa mradi kutoka kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC),
Bw. Wang Chao(aliyevaa fulana ya rangi ya karoti), wakati alipotembelea
mradi huo mapema wiki hii. Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa
asilimia 98 na litakabidhiwa kwa Serikali mapema tarehe 28 Novemba 2013. Mafundi
wakiendelea na ukamlilishaji wa daraja la Reli la Bahi-kintinku kama
walivyokutwa mapema wiki hii katika eneo la bahi mkoani Dodoma. Daraja
hilo ambalo lina tani 32 litawezesha treni la Abiria na mizigo kupita
kwa majira yote kwa uhakika. Muonekano wa daraja la reli linalojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC)
katika eneo la Bahi mkoani Dodoma. Kukamilika kwa daraja hilo
kutawezesha treni ya reli ya kati kupita kwa majira yote ya Mwaka. Aidha
daraja hilo limekamilika kwa asilimia 98.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Comments
Post a Comment