Urusi imetangaza marufuku ya vyakula kutoka kwa
muungano wa Ulaya, Marekani na nchi zingine
kadha za magharibi ambazo zilikuwa zimetangaza
vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na sera zake
nchini Ukraine.
Waziri mkuu nchini Urusi Dmitry Medvedev
aliuambia mkutano wa serikali kuwa Urusi
haitaruhusu tena uingizwaji wa Nyama, Samaki,
Matunda na bidhaa zingine kutoka mwa jumuiya ya
Ulaya, Marekani, Australia, Canada na Norway.
Medvedev amesema kuwa vikwazo hivyo vitadumu
kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amesema kuwa Urusi inatathmini kupiga marufu
mashirika ya ndege ya nchi za magharibi
yanayotumia anga ya Urusi kuingia barani Asia.
Wadadisi wanasema kuwa Urusi inategemea zaidi
chakula kutoka nje asilimia kubwa ikiwa ni kutoka
kwa nchi za magharibi.
Comments
Post a Comment