KOCHA mkuu wa zamani wa timu ya
taifa ya Tanzania, Mzalendo, Mshindo Msolla amesema walimu wa kigeni
wanaokuja nchini kufundisha klabu kubwa za ligi kuu hawasaidii
kuendeleza soka la Tanzania.
Msolla alisema makocha hawa
wanapewa mkataba wa mwaka mmoja au miwili, hivyo wanahangaika kusajili
wachezaji nyota wa kigeni ili kupata mafanikio na kuondoka, jambo ambalo
linawanyima nafasi ya kuwajenga wachezaji wazawa kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment