Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea
kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika kama
janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa kwa
dharura.
WHO imesema kuwa mataifa yalio na maambukizi
ya virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa
kudhibiti kiwango cha virusi hivyo na hivyo basi
yanahitaji usaidizi wa kimataifa.
Tangazo hilo linajiri baada ya mazungumzo ya
dharura mjini Geneva kuhusu uwezekano wa
kutuma wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili
kuudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari zaidi.
Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu mia tisa
magharibi mwa afrika .
Mataifa yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na
Sierra Leone,lakini pia visa vimeripotiwa nchini
Nigeria.
Comments
Post a Comment