Kikosi cha timu ya Mbeya City mara baada ya kupanda daraja, leo timu hiyo inapambana na Yanga jijini Mbey
SAHAU Manchester United dhidi ya Crystal Palace au Arsenal vs Sunderland. Shughuli ipo Dar es Salaam na Mbeya leo Jumamosi, unaijua?
SAHAU Manchester United dhidi ya Crystal Palace au Arsenal vs Sunderland. Shughuli ipo Dar es Salaam na Mbeya leo Jumamosi, unaijua?
Simba na Yanga zimetamba kila mmoja kwa kudai ama zao ama zetu, lakini mambo yote yatakuwa hadharani leo Jumamosi.
Vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kwa mara ya kwanza
tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi inatoka nje ya Dar es Salaam na
Simba kwa mara ya kwanza inarudi katika jiji lenye Bahari ya Hindi.
Yanga, wanacheza na timu mpya yenye hamasa kubwa
ya mashabiki mjini Mbeya ya Mbeya City kwenye uwanja chakavu wa Sokoine
huku Simba ikiwa Dar es Salaam kucheza na timu king’ang’anizi ya Mtibwa
Sugar katika uwanja wenye kapeti.
Ingawa Yanga ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye
uwanja chakavu wa Shule ya Sekondari Loyola, Dar es Salaam, Kocha wake
Ernest Brandts alisema: “Nimeuona Uwanja (Sokoine), si mzuri kabisa,
sijui mechi yetu itakuwaje.”
Mbali na hilo pia alisema wachezaji wake wana
uchovu wa safari, lakini atamkosa kiungo wake mahiri Mnyarwanda Haruna
Niyonzima ‘Fabregas’ ambaye hajajiunga na timu tangu alipokwenda kwao
Rwanda kuchezea timu ya Taifa.
Brandts alisema: “Nasikitika kumkosa mchezaji
muhimu kama Niyonzima pamoja na Hamis Kiiza ingawa wachezaji wengine
kama, Ngassa (Mrisho amefiwa na bibi yake) na Lusajo (Realintus yupo
chuo) hatupo nao kwenye safari hii ya hapa Mbeya.”
Kwa upande wa Mbeya City, kocha wa timu hiyo, Juma
Mwambusi alisema: “Mpira ni dakika 90, timu yetu ni changa na Yanga ni
wakongwe, nawaheshimu kwa hilo. Kama kocha nimejipanga kwa upande wangu
kuona tunafanya vizuri katika mechi hii.”
SIMBA VS MTIBWA
Simba ambayo ilijificha Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam, inacheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa.
Mtibwa iliifunga Simba nyumbani na ugenini kwenye
mechi za ligi msimu uliopita na wameapa kurudia hilo msimu huu jambo
ambalo limeongeza msisimko wa mchezo huo.
Wekundu wa Msimbazi wana mseto wa chipukizi kama,
Ramadhani Singano ‘Messi’, Twaha Ibrahim ‘Messi’, William Lucian
‘Gallas’ na Adam Miraji watakaosaidiwa na wazoefu kama, Abdulhalim
Humoud ‘Gaucho’, Amri Kiemba, Said Nassor ‘Cholo’ na Henry Joseph
anayecheza mechi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya misimu mitatu
alipokuwa Kongsvinger ya Norway.
Comments
Post a Comment