Israel na Palestina wamekubaliana kusitisha
mapigano tena Gaza kwa saa 72 - makubaliano
yaanza kutekelezwa Jumapili saa 6 za usiku kwa
saa za Afrika Mashariki
Wapatanishi wa Misri wamesaidia kuwezesha
makubaliano hayo kufikiwa na mapigano yakisita
kweli, Jumatatu Israel itatuma waakilishi mjini Cairo
kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya muda
mrefu katika mzozo huo.
Mwandishi wa BBC mjini Jerusalem anasema Israel
itaendelea kudai kuwa Gaza liwe eneo lisilokuwa na
silaha - na Hamas itataka Israel iache kuizingira
Gaza na iondoe vizuizi vya kuingia na kutoka.
Watu zaidi ya 20 wameuwawa tangu usitishwaji wa
mapigano wa mwisho kumalizika Ijumaa.
Comments
Post a Comment