Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine
Samba-Panza, amemteua Muislamu kuwa waziri
mkuu mpya.
Mahamat Kamoun, ambaye alikuwa mshauri
maalumu wa Michel Djotodia, kiongozi wa kundi la
wapiganaji wa Seleka, ataongoza serikali ya mpito.
Waandishi wa habari wanasema hatua hiyo ni
jaribio la kuunda serikali ya pamoja baada ya
ghasia za kidini za zaidi ya mwaka mmoja.
Tangazo hilo lilitolewa kwenye redio ya taifa na
msemaji wa rais ambaye mwenyewe ni Mkristo.
Ghasia zilizuka baina ya Wakristo na Waislamu
baada ya wapiganaji wa Seleka, wengi wao
waliokuwa Waislamu, walipomtoa madarakani Rais
Francois Bozize mwaka jana.
Comments
Post a Comment