ZIKIWA zimebakia siku nane kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Kenya Tume ya uchaguzi imejiandaa kufanya zoezi la maandalizi ya uchaguzi kwa baadhi ya vituo vilivyopo nchini humo.
Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika kituo kimoja cha kupigia kura katika kila kata yenye jumla ya kata 1,450 kwa nchi nzima.
“Vituo vitakuwa wazi kuanzia muda wa saa 06:00 hadi 05:00 suala hilo halitaaathiri chochote kuhusiana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao alisema Mutemi.
Kwa mujibu wa tume hiyo ( IEBC) alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa uchaguzi huo kwa taifa zima .
Kwa upande wake meneja mawasiliano katika tume hiyo Tabitha Mutemi alisema kuwa suala hilo litasaidia katika kupunguza kuharibika kwa kura wala kukataliwa kwa kura hizo katika kipindi cha uchaguzi.
Wapigakura hao wataandikishwa pamoja na karatasi na vifaa vingine vya kupigia kura vitatumika ili kumwezesha kila mmoja kupata nafasi ya kuchagua kati ya nafasi sita.
Nafasi hizo ni pamoja na mwakilishi wa urais, ugavana, useneta, ubunge ,upande wa wanawake pamoja na mwakilishi kwa upande wa nchi.
Aliongeza kuwa karatasi zitakazotumiwa siku hiyo zitakuwa sawa na zile zitakazotumiwa siku ya uchaguzi ambao zaidi ya wapigakura 200 watapata nafasi ya kupiga kura kwa kila nafasi hizo.
Jumla ya marais nane wameshapitishwa na tume huru ya uchaguzi kuwania kiti hicho cha Urais nchini humo
Comments
Post a Comment