Skip to main content

NYASI LEO ZA WAKA MOTO KATI YA AZAM FC DHIDI YA YANGA! KWA HABARI ZAIDI PITIA HAPA..........

AZAM FC VS YANGA: UMONY NA KIPRE BALOU WARUDI DIMBANI - KOCHA WA YANGA ASEMA ANATEGEMEA UPINZANI MKALI

YANGA inashuka leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kumenyana na Azam FC katika mchezo wa kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha wa Azam, Stewart Hall amesema kurejea kwa majeruhi Brain Omony na Kipre Balou kumempa faraja kubwa na kutamba kushinda mchezo huo na kukalia kiti cha usukani wa ligi.
"Nafikiri Omony na Balou wana mchango mkubwa kwenye timu. Uwepo wao unaongeza chachu ya timu kufanya vizuri." anasema kocha huyo.
Kwa upande wake kocha wa Yanga, Ernest Brandts amesema Azam ni moja kati ya timu bora kabisa kwenye ligi hivyo anatarajia kupata upinzani mkali.
"Azam ni timu nzuri. Ina wachezaji wenye vipaji na uwezo wakucheza kwa maelewano makubwa." anasema kocha huyo.
"Nilikuwa shuhuda wakicheza na JKT Ruvu nakushinda mabao 4-0. Nafikiri ni timu nzuri. Mchezo utakuwa mgumu. Siwezi kutabiri lolote."
Timu hizo mbili zina pointi 36 isipokuwa Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam inashika nafasi ya pili, lakini yenyewe imecheza mechi 17 wakati vinara Yanga ikicheza 16.
Endapo Yanga itapoteza mchezo huo itakuwa imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kutwaa taji hilo kwa msimu huu.
Yanga na Azam zimekutana mara tano tangu msimu wa 2011/12 katika mashindano tofauti.
Katika mechi hizo Yanga imeshinda mara mbili kama ilivyo kwa Azam FC.
Yanga iliifunga Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa fainali Kombe la Kagame na mechi ya ligi mzunguko wa kwanza kwa mabao 2-0.
Azam yenyewe iliifunga Yanga mechi mbili za ligi msimu uliopita kwa mabao 1-0 mchezo wa kwanza na ule wa marudiano ikiilaza 3-1 na kutokea vurugu kubwa baada ya Haruna Niyonzima kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Israel Nkongo ikiwa ni kadi yake ya pili ya njano kwa kosa la kumchezea rafu beki Aggrey Morris wa Azam ambaye amesimamishwa pamoja na Said Morad, Erasto Nyoni na Deogratius Minishi kwa tuhuma za kuchukua rushwa kwenye mchezo wa Simba.

Vita nyingine itakuwa kati ya washambuliaji Kipre Tchetche wa Azam na Didier Kavumbagu kama atanzishwa kikosi cha kwanza.
Jamaa hawa ndio vinara wa kufunga mabao kwenye ligi. Tchetche amefunga mabao 10 huku Kavumbagu akizamisha tisa na kuziweka timu zao katika nafasi mbili za juu.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below: