MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA NA RATIBA YA MECHI ZA WIKIENDI HII - RUVU YATAMBA KUICHINJA AZAM! kwa habari zaidi pitia hapa
MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA NA RATIBA YA MECHI ZA WIKIENDI HII - RUVU YATAMBA KUICHINJA AZAM
Maafande wa jeshi la kujenga
taifa, Ruvu Shooting ya mkoani Pwani wametamba kuwamaliza Azam Fc, Lambalamba
katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Mabatini
Mlandizi mkoani Pwani jumamosi ya wiki hii.
Ruvu Shooting wenye pointi 29 ,nafasi ya saba ya msimamo watashuka katika dimba lao la nyumbani kusaka ushindi ili kumaliza msimu huu wa ligi wakiwa nafasi nne za juu.
Ruvu Shooting wenye pointi 29 ,nafasi ya saba ya msimamo watashuka katika dimba lao la nyumbani kusaka ushindi ili kumaliza msimu huu wa ligi wakiwa nafasi nne za juu.
Akizungumza na mtandao huu, Afisa habari wa Ruvu shooting, Masau Bwire, amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda barabara huku kocha mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa “Master” akirekebisha makosa yaliyojitokeza mechi iliyopita ambayo walifungwa 1-0 na vinara wa ligi hiyo, klabu ya Yanga.
Masau alisema Azam fc jana
walishinda 3-0 dhidi ya wapiga kwata wenzao wa Tanzania Prisons hali ambayo
imewapa nguvu kubwa ya kuwania ubingwa, lakini mchezo wao wa Jumamosi
wasitarajie urahisi hata kidogo.
“Wapinzani wetu wamefanya
vizuri kombe la shirikisho kwa kuwafunga Barrack Young Controller II mabo 2-1
ugenini, jana wamepata matokeo mazuri mbele ya Prisons na wanazidi kuamsha
mizimu ya kuusaka ubingwa, sisi tunahitaji nafasi ya kushiriki hata Tusker cup
mwaka huu, hatukubali kufungwa”. Masau alitamba.
Afisa habari huyo ameongeza
kuwa mchezo uliopita dhidi ya Yanga ambao walipoteza, walistahili kushinda
kutokana na kiwango cha vijana wao, lakini walikosa nafasi nzuri za kufunga na
wapinzani wao walipata nafasi moja waliyoitumia kupata ushindi.
Masau alisema Mkwasa
anaendelea kunoa makali ya washambuliaji wake wakiwemo Hassan Dilunga, Said
Dilunga, Ernest Ernest, Ayubu kitala ili kuibuka wababe katika mchezo huo wa
kukata na shoka.
“Watanzania wanawajua vizuri
Ruvu shooting, moto tunaowasha si mchezo, tutawapiga Azam fc na baada ya hapo
tutaanza hesabu za kuwavaa Polisi Morogoro wiki ijayo”. Masu
aliongeza.
Akizungumzia malengo yao kwa
sasa, msemaje huyo amesema wapo nafasi ya saba na ponti 27 huku wakiwa na
michezo saba kibindoni, hali hii inawapa matumaini ya kufanya vizuri na kushika
hata nafasi ya nne ili kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa yaani
kombe la Tusker linaloshirikisha klabu za afrika mashariki.
Kwa upande wa Azam fc
kupitia kwa afisa habari wao Jaffar Idd Maganga wamesema kuwa mchezo
huo utakuwa mgumu sana kwao na wanauchukulia kwa umakini mkubwa sana ili
kupata pointi tatu na kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa.
Pia alisema mchezo huo
wataumia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho
dhidi ya Waliberia, Barrack Fc machi 9 mwaka huu dimba la taifa jijini Dar es
salaam.
“Sisi kila mchezo kwetu ni
fainali, katu hatudharau timu yoyote ya ligi kuu, tuna safari ndefu na
tunakabiliwa na michuano ya kimataifa, lakini tunafanya jitihada kubwa kujiandaa
kwa ajili ya mashindano yote, na jumamosi tutashinda kama jana”. Idd
alisema.
Azam fc wapo nafasi ya pili
katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 40 huku Yanga wakiwa kileleni na
pointi 48. Mabingwa watetezi simba wanabakia nafasi ya tatu na pointi 34 baada
ya kupoteza 1-0 mchezo wa jana dhidi ya Kagera sugar.
Ligi kuu kwa sasa imejigawa
katika makundi matatu, kundi la kwanza ni timu zinazowania ubingwa wa ligi kuu
kwa maana ya Yanga, Simba na Azam fc, kundi la pili ni zle zinazowania nafasi
mojawapo za juu, Mtibwa Sugar, Coastal union, kagera sugar, JKT Oljoro, Ruvu
shooting na kundi la mwisho ni zile zinazowania kukwepa mkasi wa kushuka daraja,
JKT Ruvu, Tanzania Prisons, Toto Africans, African Lyon.
Comments
Post a Comment