Februari
20, 2013 niliandika kwenye gazeti la RaiaMwema suala fulani, kufuatia
matukio ya kulaaniwa ya #Arusha Leo. Pia kufuatia mijadala inayoendelea
kuhusu #Udini nimeona vema nirejee sehemu ya Makala ile;
"Viongozi wamekuwa wakitoa kauli za kugawa wananchi. Kiongozi wa CCM kwa mfano anaposema CUF ni chama cha Waislam, anawaambiwa waislam nendeni huko ndio chama chenu. Kiongozi wa CCM anaposema CHADEMA ni chama cha kikristo, anawaambia wakristo nendeni huko ndio chama chenu. Mwanachama wa CHADEMA anapotoa taarifa kuonyesha kuwa CCM inapendelea waislamu, anadhihirisha kuwa kweli chama chake hakipendi waislamu. Viongozi wa kisiasa wanatoa kauli majukwaani bila kuzipima na kugawa wananchi. Baadhi ya taasisi za kidini zimekuwa zikutumiwa na vyama vya siasa kusambaza chuki hizi kwenye jamii.
Mimi ni Mtanzania. Taifa ambalo limejengwa kwenye misingi ya usawa na haki. Misingi ya Umoja na mshikamano. Tunu zetu ni hizo na sio dini zetu. Viongozi wanapoendelea kulea upuuzi huu wa udini Taifa litapasuka vipande vipande. Kwenye masuala ya udini watu hawaweki akili, wanaongozwa na imani. Mijadala inayoendelea sasa inatugawa sana. Lazima tukatae. Tuseme udini sio tunu ya Taifa letu, inaweza kuwa tunu ya mtu binafsi lakini Utanzania wangu ni utu, umoja, uzalendo, uwajibikaji na uadilifu.
Mtu yeyote yule anayepanda mbegu za udini asionewe aibu. Ashughulikiwe haraka sana. Wapuuzi Fulani wanasema kwa kuwa Mkuu wa Polisi ni wa dini Fulani basi ndio maana hachukui hatua. Huyu sio Mkuu wa polisi wa kwanza nchini wa dini hiyo, kuna aliyekuwepo na akaingiza msikitini askari polisi na viatu. Tusiruhusu kabisa upuuzi huu kwamba watu wenye dini Fulani hawachukui hatua dhidi ya watu wa dini zao. Vyombo vya usalama vijue, mtu anayeua ni muuaji tuna lazima achukuliwe hatua kwa uuaji wake. Tena uuaji mbaya unaojenga chuki kwa nchi yetu. Mtu anayetamka maneno ya chuki dhidi ya dini nyingine achukuliwe hatua bila kujali hadhi yake.
Mwisho hatuna namna, ni lazima Taifa liongee. Lazima tuwe na mjadala wa wazi na wa kuheshimiana kuhusu masuala ya udini na kuvumiliana kidini. Hatuwezi kuweka rehani amani ya nchi yetu kwa suala la kuswali au kusali. Badala ya kurushiana lawama, tuzungumze kwa uwazi. Makundi ya wananchi wenye kuona uonevu wa kidini waje waseme kwa uwazi na masuala hayo kujadiliwa kwa uwazi. Muhimu tupate mwafaka na kujenga Taifa imara na lenye mshikamano.
Kwa nchi yenye utajiri wa rasilimali kama yetu udini ni kichocheo tosha cha vita ya wenyewe kwa wenyewe na migogoro isiyokwisha. Ni lazima tuchukue hatua sasa.
Tuache unafiki wa kunyoosheana kidole. Kila mtu atazame nafsi yake na aseme ukweli wake kwa uwazi kabisa. Tusifukie uchafu chini ya kapeti.

Comments
Post a Comment