Skip to main content

HIZI HAPA PICHA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa
..... bodaboda.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
 
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume .
 Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.
 
Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.
“Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,” alisema Josephine kwa uchangamfu.

Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.

Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...