Skip to main content

HIZI HAPA VIDEO YA WEMA SEPETU AKIWAPOROMOSHEA MATUSI MAZITO WAFANYAKAZI WAKE WA NDANI


STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi.  

Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa.......
mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.  

Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua tatizo. 

Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.

Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.

Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.  

Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na kuanza kutoa mkong’oto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele yake.

  Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni isiyoandikika  kutokana na ukali wake. 

  “My friend ninyi ni mabogasi kabisa, nawaambia mtaozea Segerea, mnafanya nini hapa ninyi wa…(tusi) au mna…(tusi kali). 


 “Ninyi ni …(tusi kubwa likihusisha mama zao), mnakaakaa tu hapa wa…(tusi tena), mnajua bei ya power window? Mnadhani hili ni Toyota? Kwa taarifa yenu hili ni Lexus …(tusi) zenu,” alisikika Wema akitumia lugha ya matusi ambayo asilimia kubwa hayaandikiki kwa namna yoyote kutokana na kupitiliza.

Wema aliendelea kuwakimbiza ndani ya fensi akiwapiga huku sauti ya Martin Kadinda (yule meneja wake) ikisikika, ‘Mwache ataruka ukuta, nenda karipoti polisi’.

  Huku akiwa mbogo, Wema alimgeukia mmoja wa mbwa wake aitwaye Fiona na kumuwashia moto huku akimmwagia mitusi:

“Na wewe Fiona unakaa hapo hapo unamuuzia nani sura badala ya kulinda mlinzi, sipendi mambo ya ki… (tusi) 


Mkurugenzi huyo wa kampuni ya kufyatua filamu ya Endless Fame Production alikwenda mbali na kuwatuhumu wafanyakazi hao kuwa kuna uwezekano wanatumiwa kumhujumu akiahidi kuwakomesha.

“Mnatumwa mnapewa pesa ili mnifanyie hivi…gari litaibiwaje power window likiwa ndani na ninyi mkiwepo? Wa…(tusi) sana ninyi,” alisikika msanii huyo.  

Katika hali ya kushangaza, badala ya kumuwashia moto mlinzi anayehusika na usalama nyumbani hapo, Wema ‘alidili’ na wafanyakazi wa ndani tu huku mlinzi naye akishindwa kumuamulia na kubaki kumtazama tu namna alivyokuwa akikimbizana na wafanyakazi hao.

 Kwa upande wao majirani walikuwa wakila chabo na kusikitishwa na mvua ya matusi aliyokuwa akiitoa msanii huyo ambaye ni kioo cha jamii.

  “Jamani jamani, hivi hajui tuna watoto wadogo ambao hawastahili kusikia matusi makubwa kama anayomwaga? “

Ukweli Wema anatusikitisha sana kwa sababu watoto wanajifunza nini kutoka kwake?” alihoji mmoja wa majirani hao aliyeomba hifadhi ya jina ili na yeye asije akawashiwa moto na msanii huyo

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...