Mwanahamisi Majube amelala katika kitanda cha hospitali moja ya umma (jina linahifadhiwa) ikiwa ni saa chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa kujifungua.
Analia na kuugulia kwa uchungu, akilalamikia maumivu makali ya tumbo.
Kwa sababu hiyo, anamwita daktari akimweleza kuwa
anahisi kuna kitu tumboni mwake na kinamuumiza mno, lakini daktari
anamjibu kuwa ..........
maumivu hayo yatatulia.
maumivu hayo yatatulia.
“Nisaidieni nitakufa kabla ya kumwona mtoto wangu, naumwa daktari, nakufa jamani,” anasema Mwanahamisi.
Anapoendelea kuita, wakunga ndani ya wodi hiyo
wanaibuka na kumjibu: “Acha kudeka, ulifikiri kuzaa ni kama kucheza
kamari. Nyamaza, unawapigia kelele wenzako.”
Anaendelea kuita kwa zaidi ya saa lakini bila
msaada wowote na baada ya kulia kwa muda mrefu, anatupa miguu huku na
kule…ananyamaza, kisha anatulia. Kumbe… Mwanahamisi amekata roho!
Mwanahamisi ni miongoni mwa wanawake wengi nchini
ambao hukumbana na vifo vya kuepukika wakati wa kujifungua au muda
mfupi baadaye.
Vifo hivyo, vingi vinasababishwa na uzembe wa
madaktari, huduma dhaifu, ukosefu wa vifaa na sababu nyingine
zinazozuilika wakati wa kujifungua.
Pamoja na uchungu wa kujifungua anaoupata
mwanamke, ukosefu wa vifaa tiba, maumivu mengine huyapata toka kwa
baadhi ya wahudumu wa afya.
Hali hiyo imesababisha baadhi ya wanawake, hasa
wale wanaojiweza kukimbilia katika hospitali binafsi ambapo wanapata
huduma bora zaidi.
Hata hivyo, ni wanawake wachache nchini wenye
uwezo huo na zaidi ya asilimia 80 wanategemea hospitali za Serikali
ambazo baadhi, ndizo zenye changamoto.
Katika mdahalo wa afya ya uzazi uliondaliwa na Dk
Tausi Kida na Riziki Pansiano, wadau walikiri kuwa kuna matatizo mengi
yaliyowakumba wanawake wakati wa kujifungua, kubwa likiwa rushwa na
matusi.
Comments
Post a Comment