TV zingine zinaweza kuenea ukuta mzima wa nyumba, na inaweza.........
kukaa katika sakafu, au kuna zingine ambazo zimenyooka (flat) na zinaweza kubandikwa ukutani. Televisheni inaweza kuonyesha picha kutoka sehemu mbalimbali. Cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kutumia kidaka mawasiliano au antenna (au aerial), hii itaonyesha maonyesho yote yanayorushwa na kituo cha matangazo ya televisheni.
Vituo vya TV vinaweza kuwa mbali kabisa lakini bado matangazo yake yanapatikana kama antena ya kurusha mawimbi yake iko katika umbali wa kilomita 50 hadi 150. Teknolojia mpya zaidi ni kutumia vyombo vya angani kama antena ya kurusha mawimbi haya duniani. TV pia inaweza kuonyesha filamu kutoka katika VCD na DVD au VCR yaani tepu za kawaida. Cable TV na Satellite TV zinaweza zikatoa huduma nyingi ya vipindi vya TV kwa mara moja na vilevile kuvirusha hewani. Michezo mingi ya Video huunganishwa katika TV ili uweze kuona kile unachokicheza. Kuna baadhi ya tarakilishi au kompyuta ambazo unaweza kutumia TV kama kioo cha kufanyia kazi zako (kiwambo) au kwa jina lingine monitor.
TV zote zina kiwambo ambacho kinaonyesha picha. Kabla ya miaka ya 1970 TV zilikuwa hazina rangi ( yaani "black and white"), ambazo zilikuwa zinafanya kila kitu kionekane cha rangi ya kijivu. Lakini kwa sasa karibuni TV zote zinaonyesha na rangi. Kawaida ya viwambo vingi (kioo au vioo) vingi huonyesha kuwa vina kona ya mzunguko, lakini kwasasa vioo vingi hutengenzwa kwa kunyooka na zina ncha pembeni.
Kabla ya miaka ya 1990, TV zote zilikuwa zikitengenezwa kwa umbo moja-zilikuwa kubwa kidogo na kisha zilikuwa ndefu. Kwa mfano, kama kioo kilikuwa cha urefu wa inchi 3, basi lazima kitakuwa na upana wa inchi 4. Au kama kioo kina urefu wa cm 30, lazima kitakuwa kina upana wa cm 40.
Umbo la TV za kisasa linazidi kuwa maarufu na kupata wapenzi wengi zaidi kila siku ziendapo. TV zenye kioo cha upana mkubwa wa mstatili huonekana vizuri katika runinga kubwa (theatre screen) na pia inapendeza wengi zaidi. Hizi huziita kioo kipana (au kwa kiing: widescreen). Endapo TV ya kioo kipana ina urefu wa cm 30, basi lazima itakuwa ina upana wa cm 53. Ili ifanye kazi vizuri, uonyeshaji wa TV pia unatakiwa ujengwe kwa namna ya upana yaani 'widescreen'. Kioo kipana kinaweza kubadilishika kwa ukubwa wowote unaoutaka, lakini swala la umbo linabaki kuwa vilevile kama lilivyo (Widescreen).
Comments
Post a Comment