Skip to main content

HIVI NDIVYO AGNES MASOGANGE ALIVYOKAMATWA




ZIMEPITA siku 16 tangu Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kunaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park nchini Afrika Kusini, mapya yameibuka kuambatana na tukio hilo, Risasi Jumamosi linakupasha.

Chanzo chetu cha ndani kilichoongea na...........
paparazi wetu juzi jijini Dar, kimesema neno kwa neno, hasa matukio ya siku nne wakati staa huyo akijiandaa kuondoka nchini. Masogange aliondoka Julai 5, 2013.
JULAI 2, 2013
Masogange alipika pilau nyumbani kwake, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na kuwaalika watu mbalimbali, wakiwemo kaka zake ambao majina yao hayakupatikana mara moja.
Katika ‘hafla’ hiyo, Masogange alisema amejisikia kula pamoja na watu hao ili kutimiza furaha ya moyo wake. Hakusema ana furaha gani.

JULAI 3, 2013
Inadaiwa Masogange siku hiyo aliazima gari la mdau wake mmoja (jina tunalo) na kuwa nalo kwa saa kadhaa.
Safari yake kubwa ilikuwa Sea View Hotel, jijini. Siku hiyo staa huyo hakuwa akipokea simu asizozijua. Wale aliowajua aliwaambia ana mazungumzo nyeti na mtu hotelini hapo, hivyo wapige baadaye.

JULAI 4, 2013
Masogange aliposti picha kwenye Instagram akiwa yeye na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ wakila ‘bata’. Aliandika maneno mbalimbali kama; ‘libeneke la bata litaendelea nikirudi.’ Hakusema anakwenda wapi na lini atarudi.

KUHUSU ‘UNGA’
Chanzo kilisema: Nijuavyo mimi mtu akiwa na mabegi mengi yenye madawa ya kulevya na anataka kusafiri nayo, yanatangulia uwanja wa ndege. Hivyo naamini mzigo ulipelekwa uwanja wa ndege siku hiyo.

ALIKWENDA SALUNI
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, pia siku hiyo jioni alikwenda saluni moja iliyopo Sinza Madukani, Dar. Jina halijajulikana.

JULAI  5, 2013
Shuhuda anasema saa 4:06 asubuhi, Masogange alifunga safari kwenda uwanja wa ndege akiwa ameongozana na Melisa Edward ambaye anadaiwa kukamatwa naye siku hiyo.

MABEGI YANAYOTUMIKA KUBEBEA ‘UNGA’
Kingine ambacho kimesemwa, mabegi yanayotumika kubebea ‘mzigo’ ni spesho kwa kazi hiyo ambapo ndani yana zipu mbili.
“Mabegi yaliyotumika siku hiyo si haya ya kawaida yanayouzwa na machinga, unajua wabeba unga wanatumia mabegi yanayojulikana kwa jina la Hand Curter, juu yana zipu moja kubwa, ndani kuna zipu mbili ambazo wewe kuziona ufanye kazi.
“Begi moja linauzwa shilingi laki nne (400,000). Kama uwanja una zana duni za kukagulia, hawawezi kuona unga ndani,” alisema sosi huyo.

MZIGO ULITOKEA BARA LA ASIA
Kwa mujibu wa maelezo ya mtu mwingine, mzigo aliokamatwa nao Masogange unadaiwa kuingia Bongo Juni 29, 2013 ukitokea nchi moja iliyopo Bara la Asia (jina tunalo).
“Sina uhakika na lini mzigo huo uliingia au safari hiyo aliipanga, lakini kumbukumbu zangu zinaniambia mzigo uliingia Bongo Juni ishirini na tisa, mwaka huu, ukitokea nchini …(anaitaja jina),” alisema mtu huyo.

AKIPATIKANA NA HATIA ADHABU NI HII
Habari kutoka chanzo chetu kimoja nchini Afrika Kusini, mtu anayepatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya kwa kuuza au kubeba huhukumiwa kifungo cha maisha au kifungo cha miaka 20.

MADAWA YAMEPELEKWA KWA MKEMIA
Aidha, kuna habari kwamba baada ya serikali kuyadaka madawa hayo, yamepelekwa kwa mkemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi zaidi na majibu yatatolewa Agosti, mwaka huu.

DHAMANA IPO WAZI, NANI AMUWEKEE?
Habari mbaya ni kwamba, dhamana ya Masogange na mwenzake iko wazi mahakamani lakini watu wa kwenda mstari wa mbele kumuwekea ndiyo wamekuwa wakiingia mitini.
“Huku dhamana iko wazi, ila kila mtu anaonekana kukwepa kumdhamini. Sijui watu wanadhani atatoroka? Lakini nijuavyo mimi hawezi kutoroka kwa sababu paspoti yake inashikiliwa na serikali,” alisema mnyetishaji wetu aliye nchini humo.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...