Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji kupokea miili saba ya wanajeshi wa Tanzania waliouawa Darfur, Sudan, Julai 13, mwaka huu.
Miili ya wanajeshi hao saba iliyowasili jana ni
............ SajIni Shaibu Sheha Othman, Koplo Osward Paulo Chaula, Koplo Mohamed Juma Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Peter Werema na Private Fortunatus Msofe.
............ SajIni Shaibu Sheha Othman, Koplo Osward Paulo Chaula, Koplo Mohamed Juma Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Peter Werema na Private Fortunatus Msofe.
Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya Jeshi la Kulinda
Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), kusini mwa Darfur na walitoka katika
vikosi vya, 42KJ Chabruma, Songea, 44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ
Ngerengere, 94KJ cha Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao
Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa wanajeshi hao waliuawa na kikundi
cha waasi cha Janjaweed kinachoungwa mkono na serikali ya Sudan, huku
wengine 19 wakijeruhiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walikuwa
wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yametekwa na kundi hilo.
Hali ilivyokuwa
Baada ya miili hiyo kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Jeshi saa 10:40 jioni na ndege ya Antlantis iliyotolewa na
Umoja wa Mataifa(UN), mamia ya watu waliokuwapo uwanjani hapo
walionekana kuingiwa na huzuni baada ya kuona miili ya marafiki, ndugu
na jamaa zao ikishushwa kwenye ndege hiyo.
Baada ya ndege hiyo kuwasili, viongozi wakuu wa
Serikali pamoja na wambolezaji wengine waliisogelea ndege hiyo kwa ajili
ya kupokea miili ya wanajeshi hao.
Miili hiyo ilishushwa na kuingizwa kwenye magari
saba ya jeshi, na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi la Lugalo kwa
ajili ya kuhifadhiwa.
Wanajeshi hao wanatarajiwa kuagwa kesho Jumatatu
katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi Upanga, baadaye miili hiyo
itasafirishwa kwenda kuzikwa katika maeneo yaliyotengwa na familia zao.
Waombolezaji
Baadhi ya ndugu wa marehemu waliofika kwenye viwanja hivyo walisema kuwa walikuwa wakiwategemea sana ndugu zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema mara
baada ya kupata taarifa za vifo hivyo, walishtuka na kutoamini
kilichotokea huku wakieleza kuwa walikuwa wanawasiliana nao mara kwa
mara wakati wakiwa Darfur.
Comments
Post a Comment