Wizi huo wa ajabu ulitokea Julai 18, mwaka huu,
ambapo majambazi hao walivunja kituo hicho ambacho ndani yake kuna Ofisi
ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC).
Mwanza. Majambazi wamevunja ofisi za Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mwanza na kuiba mali mbalimbali vikiwemo vielelezo vya watuhumiwa walio na kesi mahakamani.
Wizi huo wa ajabu ulitokea Julai 18, mwaka huu,
ambapo majambazi hao walivunja kituo hicho ambacho ndani yake kuna ..........
Ofisi ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC).
Ofisi ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC).
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zilibaini kuwa
majambazi hao walivunja ghala la vielelezo vya washtakiwa, chumba cha
ghala la vipuri vya magari ya polisi, zikiwemo ofisi za Wapelelezi wa
Makosa ya Jinai na Waendesha Mashtaka.
Majambazi hao wanadaiwa kuiba majalada ya kesi,
begi lililokuwa na vielelezo vya washtakiwa, kompyuta ndogo mbili
(Laptop) za ushahidi na kutoweka.
Wizi huo uliotokea usiku na kubainika asubuhi,
ambapo watu hao ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa waliweza
kufanikiwa kuingia ndani ya ofisi hizo za polisi, kwa kuvunja madirisha
mawili ya chumba cha ghala la ofisi za Mkaguzi wa Elimu Kanda ya Ziwa
ambazo zinapakana na Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati cha Jijini Mwanza,
kisha kufanikisha wizi huo.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Jeshi la
Polisi zinaeleza kwamba wizo huo ambao ulilenga ofisi ya vielelezo na
mashtaka, ulipangwa kwa umakini na kutekelezwa bila ya polisi waliokuwa
zamu usiku huo kubaini lolote.
Kwa mujibu wa maelezo wezi hao inadhaniwa ni watu
wenye uzoefu na jengo hilo, wakiwa na nia ya kuchukua vielelezo
mbalimbali pamoja na mafaili muhimu ya kesi kubwa.
Hili ni tukio lingine kubwa kutokea kwa Jeshi la
polisi Mkoa wa Mwanza sambamba na tukio la kuuawa kwa aliyekuwa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Oktoba 13, mwaka jana ambaye
alipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi saa nane usiku
wakati akitoka katika kikao cha harusi.
Kauli ya Kamanda Mangu:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Evarist Mangu,
amethibitisha kutokea kwa wizi huo na kusema jeshi lake linafanya
uchunguzi wa kina kubaini waliohusika, na kusisitiza kuwa kama ni askari
wake ama watu toka nje hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema wezi hao waliingilia katika ofisi ya
Ukaguzi Elimu Kanda ya Ziwa ambako walivunja madirisha mawili, moja
likiwa ni kuingia ndani ya ghala la ofisi za elimu na dirisha lingine la
kutokea nje ya ghala hilo, kisha kuvunja dirisha la ndani ya majengo ya
polisi na kufanikisha wizi huo.
“Wezi hao walipiga jeki nondo za madirisha hayo,
hivyo kung’oka na kuingia ndani kisha kwetu, walianza kuingia katika
ghala la polisi la kuhifadhia vifaa vya ofisi vya Jeshi la polisi,
lakini inaonekana walikosa cha kuiba, huko walipanda darini na kutokea
katika chumba kingine nako hawakuiba, lakini katika chumba cha vielelezo
ambako walikuta begi lililokuwa na nguo za vielelezo pamoja na kompyuta
ndogo mbili, Lap Top, ambazo walitoweka nazo,” alieleza Kamanda Mangu
Comments
Post a Comment