Skip to main content

SOMA HAPA WARAKA WA KALA JEREMIAH YA KUMPIGIA KAMPENI LOWASSA....ANADAI LOWASSA NI JEMBE



Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini.


Usome waraka wake huo wote;
Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond.


Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli........... mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa.


Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisiasa, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu.


Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo unaoitwa ‘Azimio la Arusha’ ambao upo kwenye album yangu ya Pasaka ambayo iko sokoni tokea mwaka jana.

 Katika wimbo huo wa Azimio la Arusha niliandika mistari ifuatayo, walipiga dili waka msakizia Lowassa ili kuficha siri kali.


Niliandika mstari huu baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa mheshimiwa ni kiongozi bora sana na hasa kwa uamuzi wake wa kujiuzulu bila shinikizo kubwa na wakati kwa nafasi aliyokuwa nayo ya uwaziri mkuu alikuwa na uwezo wa kugoma kujiuzulu na hasa kwa kuwa hakuwa fisadi kama ilivyosemwa.


Mwezi wa tatu mwishoni mwaka huu nilitoa wimbo unaokwenda kwa jina la Karibu Dar ambako nilisema ‘Dar es Salam ingekuwa nchi rais angekuwa Lowassa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa’, hapa nilikuwa namaanisha kuwa watu wengi wanaoishi Dar wanawahi kujua mambo ya wanasiasa kwa kuwa wanasiasa wanaishi huku lakini pia watafiti wengi wa mambo ya kisiasa wanaishi huku kwa hiyo ni rahisi zaidi kuujua ukweli mapema.


Naamini kuondoka kwa Lowassa kwenye uwaziri mkuu kumezorotesha maendeleo ya taifa kwa kiasi fulani.


Ndugu zangu watanzania ni wazi kuwa Lowassa ni jembe tena jembe la kazi kumbukeni bila Lowassa kusingekuwa na shule za kata Tanzania,na angeendelea kuwepo madarakani alikuwa na mpango wa kuanza mchakato wa zahanati za kata, ikumbukwe pia Lowassa ndiye aliyesimamia ujenzi wa chuo cha udom tena kwa pesa za kitanzania bila kuombaomba vimikopo.


Mradi wa maji kutoka Mwanza kwenda Shinyanga ni kazi ya Lowassa, zipo kazi nyingi ambazo nikizitaja zote naweza kujaza ukurasa.


Nachojaribu kusema hapa ni kwa kuwa mimi ni msanii na ni kioo cha jamii ningeomba wewe mwanajamii chukua hatua ya kufanya uchunguzi binafsi kuhusu Lowassa, bila kufuata mkumbo wa kisiasa naamini utakubaliana na mimi kuwa Lowassa ni jembe.
 
Mimi huwa napenda kusoma vitabu vya wanaharakati na kuna kitabu kimoja nilikipitia cha mwanaharakati kutoka Italy aitwae Niccolo Machiavelli ambaye alizaliwa mwaka 1469 na kufariki 1527. 

Katika enzi za uhai wake aliwahi kuandika vitabu kadhaa lakini kati ya vitabu hivyo kitabu kiitwacho ‘The Prince’ ndicho kilimpa heshima kubwa sana kwa kuwa aliikosoa serikali ya kifalme ya kipindi hicho kitu ambacho hakikuwa rahisi kwa mtu kufanya hasa ikikumbukwa kuwa enzi za ufalme zilikuwa enzi za ubabe.


Katika maneno kutoka kwenye kitabu hicho ambayo ninge penda kukushirikisha wewe ndugu yangu Mtanzania ni maneno yafuatayo,machiavelli aliandika hivi: 

‘Kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu, na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.



Atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendelea kukumbukwa. Kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.’


Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika na Machiavelli kwenye The Prince, kitabu ambacho kilimpelekea kuitwa na mfalme na kupewa nafasi ya juu ya uongozi katika serikali hiyo ya kifalme.


Kwa maoni yangu nadhani taifa letu limepitia vipindi vigumu kadhaa na kwa maneno ya Bwana Machiavelli nadhani kiongozi anayefaa ambaye anaweza akachukua maamuzi magumu na ambaye hawezi kuwa chini ya sauti ya mtu mwingine ni mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa.

 
Kuna watu wanasema nimenunuliwa sijui nimepewa pesa. Mimi kama mkristo niliyebatizwa kwa maji mengi naapa sijawahi kumjua Lowassa kuonana naye wala kuwasiliana naye zaidi ya kumuona kwenye TV.


Ila nimejisikia kuongea haya kwa sababu watu wengi tunafuata yanayosemwa na wanasiasa hatuangalii nani aaaweza akafanya nini kwenye taifa letu.Mimi nina mashabiki na mashabiki wangu ndiyo maboss wangu nitafurahi sana kama maboss wangu watapata maisha bora na kwa kupitia maisha bora ya mashabiki zangu na mimi nitakuwa na maisha bora.


Amini hakuna mwana siasa anaweza kumnunua Kala Jeremiah kwa senti ingekuwa hivyo ningeshanunulika miaka hiyooo. Narudia tena Lowassa ni jembe.


Wanaosema nimehongwa mwaka jana wakati naenda studio kurecord wimbo wa Azimio la Arusha ambao ndo ulikuwa wimbo wangu wa kwanza kumtetea Lowassa, nilienda studio kwa daladala. Mwaka huu mwanzoni wakati naenda studio kurecord ‘Karibu Dar’ niliendaaa studio kwa daladala.


Mpaka sasa napost post hii mimi ni msanii bora wa hip hop lakini sina gari, wanaonifahamu kwa karibu wanalijua hilo. Je kama fisadi kaninunua kanilipa elfu kumi au?

Najua mtakuja kuelewa baadae nafanya hivi kwa ajili ya kulilia wananchi maskini wenye ndoto za kuishi maisha bora.
Halafu Lowasda sio mtu wa kwanza mimi kumsifia. 


Nilishaawahi kuwasifia Dr Slaa, Zitto Kabwe,Mwakiembe, basi ingekuwa ninakusanya hela basi ningekuwaa milionea mkubwa sana kwa sasa.

Comments

Popular posts from this blog

ANGALIA VIDEO YA MWANAMKE AKIZINI NA CHUPA YA SODA YANASWA

 Katika  hali  ya  kushangaza  na  kuashiria  miisho  ya  dunia, binti  mmoja  amenaswa  " live " akifanya  mapenzi  na  CHUPA YA SODA. Katika  video  hiyo, binti  huyo  anaonekana  akitoa  ushirikiano  wa  kutosha  mithili  ya .............

HUYU NDIYE ALIIYELAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI NA MBWA PAMOJA NA FARASI KWA AJILI YA PESA.

When the Internet first came to the continent of  African society,most people were  very pleased with it because it reduces stress of communication with love around the world,it also serve as productive purposes like communication.It served many people for chatting, sending mails and even business. As the time passed by many ladies discovered that they could use the internet to find a chat friend or a life partner.Some girls have greatly benefited just by using the internet to find their dream marriages or relationhsips. Others have fallen into traps in the West and wish they would never have known what the internet was.This is the case of one Cameroonian,Elvire Axelle Tchamakoua. Continue....... SEE HOW IT ALL HAPPEN.... Axelle is pr00stit-te who is pimped to various men by her main man Jean Claude(French Businessman).She did not mind serving her customers from the front or from behind.The use of condoms during her encouters was the allowed as it b

HAYA NDO MANENO YA KUMPANDISHA hisia MPENZI WAKO UMPENDAE!!!!!

                                       Inawezekana wengi wetu tukawa tunayatumia bila kujua kwamba tumekusidia kuyatumia. Haya ni maneno au kauli ambazo mume/mke anaweza mwambia mwenza wake kama ishara ya kumpandisha "nyege" kabla ya kuanza  kufanya mapenzi. Wawili hawa wanaweza wakawa sehemu tofauti tofauti, mfano mume yupo kazini lakini anakaribia kurudi nyumbani, mke ukaanza "kumcharura" mumeo kwa kauli mbali mbali aidha kupitia sms au kwa kumpigia simu, ingawa kupitia sms ndo inasisimua zaidi! Hapa najua naongea na watu wazima, sina haja ya kuandika zaidi maneno yenyewe lakini kila mmoja ni mjuzi wa tabia na vitu ambavyo mwenza wake anavihusudu hasa mkiwa kitandani, mfano" Baby ukirudi leo nataka unipindishe pale katika dressing table kama ulivyonifanyia jana, na leo nimevaa lile gauni ulipendalo na zile bikini mpya, dont be late my love" Maneno haya kwa anayejua mapenzi na anampenda mkewe ni lazima huko alipo "Jogoo" awike kidog