WAKAZI
wa mikoa ya jirani tayari wameanza kumiminika jijini Dar kwa ajili ya
kushuhudia Tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7, mwaka huu
katika Uwanja wa Taifa.
Gumzo zaidi linalozungumzwa na mashabiki hao ambao wengi wao wamesema wanatokea Mikoa ya Morogoro, Tanga, Iringa na Dodoma ni kuwaona wabunge wa Simba na wale wa Yanga watakaposhuka dimbani kucheza soka huku baadhi yao wakishiriki katika mapambano ya..........
ndondi dhidi ya waigizaji.
Kwenye eneo la ndondi, Mhe. Halima Mdee atapigana na Jacqueline
Wolper, Mhe. Zitto Kabwe na Vincent Kigosi ‘Ray’, Mhe. Ester Bulaya
atavaana na Aunt Ezekiel huku balaa zaidi likitarajia kuandikwa na
mabondia Patrick Amote (Mkenya) atakayevaana na Thomas Mashali
(Mtanzania) huku Mkenya Shadrack Muchanje akipigana na Francis Miyeyusho
(Mtanzania).
“Nimetoka Tanga hadi Dar kwa ajili ya kushuhudia tukio hili kubwa la historia, navuta picha pale jukwaani nimuone Mhe. Zitto Kabwe akizichapa na Ray na pale wabunge wa Simba watakapojitupa uwanjani kucheza soka,” alisema Ally Juma, mkazi wa Tanga.
Mratibu wa tamasha hilo lenye lengo la kuchangia Mfuko wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewahakikishia mashabiki waliotoka mikoa ya jirani pamoja na wenyeji, burudani itakwenda kama ilivyopangwa na ulinzi wa kutosha.
“Ni tamasha kubwa, mbali na mechi za wabunge na ndondi, kutakuwa na burudani ya Prezzo, Diamond, Wanaume Halisi, Bendi ya Mlimani Park, Jahazi, Wanaume Family na H. Baba, mechi za mpira wa miguu kati ya Bongo Fleva na Bongo Movie.
“Hayo yote yatafanyika chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, mbwa, farasi, Ninja zaidi ya 60 na mabaunsa wasiopungua 50. Niwahakikishie mashabiki wataondoka uwanjani salama salmini,” alisema Abby Cool na kuongeza:
“Mwigizaji Jacob Steven ‘JB’ amesema anamhitahitaji Mhe. Idd Azzan kwenye ndondi hivyo kama mbunge huyo ataridhia, watavaana ulingoni ambapo JB ameapa kumtandika mheshimiwa huyo ndani ya sekunde 35.”
Viingilio vya tamasha hilo ambalo pia litahusisha mechi za wanafunzi wa Sekondari za Jitegemee na Makongo, vitakuwa ni shilingi 20,000 kwa V.I.P, 10,000 viti vya bluu na 5,000 viti vya kawaida.
Gumzo zaidi linalozungumzwa na mashabiki hao ambao wengi wao wamesema wanatokea Mikoa ya Morogoro, Tanga, Iringa na Dodoma ni kuwaona wabunge wa Simba na wale wa Yanga watakaposhuka dimbani kucheza soka huku baadhi yao wakishiriki katika mapambano ya..........
ndondi dhidi ya waigizaji.
“Nimetoka Tanga hadi Dar kwa ajili ya kushuhudia tukio hili kubwa la historia, navuta picha pale jukwaani nimuone Mhe. Zitto Kabwe akizichapa na Ray na pale wabunge wa Simba watakapojitupa uwanjani kucheza soka,” alisema Ally Juma, mkazi wa Tanga.
Mratibu wa tamasha hilo lenye lengo la kuchangia Mfuko wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewahakikishia mashabiki waliotoka mikoa ya jirani pamoja na wenyeji, burudani itakwenda kama ilivyopangwa na ulinzi wa kutosha.
“Ni tamasha kubwa, mbali na mechi za wabunge na ndondi, kutakuwa na burudani ya Prezzo, Diamond, Wanaume Halisi, Bendi ya Mlimani Park, Jahazi, Wanaume Family na H. Baba, mechi za mpira wa miguu kati ya Bongo Fleva na Bongo Movie.
“Hayo yote yatafanyika chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, mbwa, farasi, Ninja zaidi ya 60 na mabaunsa wasiopungua 50. Niwahakikishie mashabiki wataondoka uwanjani salama salmini,” alisema Abby Cool na kuongeza:
“Mwigizaji Jacob Steven ‘JB’ amesema anamhitahitaji Mhe. Idd Azzan kwenye ndondi hivyo kama mbunge huyo ataridhia, watavaana ulingoni ambapo JB ameapa kumtandika mheshimiwa huyo ndani ya sekunde 35.”
Viingilio vya tamasha hilo ambalo pia litahusisha mechi za wanafunzi wa Sekondari za Jitegemee na Makongo, vitakuwa ni shilingi 20,000 kwa V.I.P, 10,000 viti vya bluu na 5,000 viti vya kawaida.
Comments
Post a Comment