Skip to main content

Kumbe Operesheni Kimbunga Haikuondoa Wakimbizi Nchini


1994_Crisis_Goma_36882-c-Roger-Job

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Operesheni Kimbunga haikuondoa Wakimbizi nchini kama ilivyoripotiwa na baaadhi ya Vombo vya Habari vya hapa nchini na vya nje.
Ifahamike kuwa zoezi hili limehusisha Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) ili kuhakikisha kuwa wakimbizi hawahusishwi katika zoezi la kuondoshwa nchini.
Kwa mujibu wa tafsiri iliyotolewa na Mkataba wa Kimataifa wa mwaka 1951 kuhusu hadhi ya Wakimbizi, Mkimbizi ni mtu anayekimbia nchi yake kwa hofu ya maisha yake kuwa hatarini kwa sababu za  kikabila, dini, utaifa, uanachama wa chama cha kijamii au kisiasa na kufuata hifadhi katika nchi nyingine.
 Mkimbizi anapokimbilia katika nchini nyingine kuomba hifadhi ana haki ya kupewa hifadhi na kuhakikishiwa usalama wake. Pia ana haki ya kupokelewa na kutorudishwa katika nchi ambayo ameikimbia.
Hivyo , kutokana na Mkataba huo, Tanzania wakati inatekeleza Operesheni Kimbunga haikumgusa mkimbizi.
Aidha, ieleweke kuwa yapo mazingira ambapo hadhi ya mkimbizi hukoma pale ambapo suluhisho la kudumu la matatizo ambayo yalimfanya mkimbizi kukimbia nchi yake limepatikana na hivyo mkimbizi mwenyewe kutaka kurudi nchini kwake kwa hiari ama pale mkimbizi anapohamishiwa kwenye nchi ya Tatu kwa makubaliano maalum na pale ambapo mkimbizi anapewa uraia  au ukaazi wa nchi  iliyompatia hifadhi.
Hivyo basi, mkimbizi anaweza kuwa mhamiaji haramu pale ambapo hakurudi katika nchi yake kwa hiari baada ya kupatikana suluhisho kwa matatizo yaliyosababisha kukimbia ama hakupata fursa ya kwenda nchi ya Tatu na hakuomba Uraia au ukaazi wan chi iliyokuwa inampa hifadhi.
Ieleweke kuwa Mkimbizi ambaye alirudi nchini kwake kwa hiari yake na baadaye kuamua kurudi katika nchi iliyokuwa inamhifadhi hawezi kuendelea kuwa na hadhi ile ile ya ukimbizi . Mtu huyu anatakiwa kufuata Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya 1995. Iwapo ataishi nchini bila kufuata sheria hiyo atahesabika kuwa mhamiaji haramu.
Inawezekana kuna watu ambao hadhi yao ya ukimbizi imekoma na wanaishi nchini isivyo halali wakakumbwa na  Operesheni Kimbunga na kudai kuwa wao  ni wakimbizi.
 Juhudi za Serikali za kuwataka wahamiaji haramu kuhalalisha ukaazi nchini kwa hiari
Kwa vipindi tofauti, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji iliendesha zoezi la kuhamasisha watu wanaoishi nchini isivyo halali kurudi nchini kwao kutokana na hali ya usalama katika nchi hizo kuimarika. Aidha, kwa waliotaka kubaki na kuendelea  kuishi nchini walielekezwa kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.
Utafiti uliofanywa na Mradi wa Kimataifa wa kushughulikia masuala ya kiuhamiaji  ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaoongozwa na Prof. Boneventure Rutinwa  2006/2007 katika mkoa wa Kagera  unaonyesha kuwa Wilaya ya Karagwe pekee Inakadiriwa kuwa na wahamiaji haramu 30,850 lakini pamoja na kuhamasishwa kuhalalisha ukaazi wao, watu 2,000 pekee walifuata taratibu walizoelekezwa na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji ili kuhalalisha ukaaji wao nchini.
Pamoja na juhudi zote za Serikali za kuhamasiha wahamiaji haramu kuhalalisha ukaazi wao nchini bado hawakufuata taratibu na badala yake utafiti unaonyesha kuwa waliendelea kuingia na kuhamia katika wilaya nyingine mfano Biharamulo na maeneo mengine.
Taarifa hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Septemba 20,2013, Biharamulo, Kagera. Kwa maelezo zaidi Email: zamaradikawawa@yahoo.com.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below: