



………………………………………………………………………….
Taasisi ijulikanayo kwa jina la “Inmate Rehabilitation and Welfare Services Tanzania” (IRaWs – T) ya Jijini Dar es Salaam imetoa Mafunzo Maalum kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza juu ya namna ya kushirikiana katika kukabiliana na Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu Magerezani.
Akiongea katika Mafunzo hayo Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa ameyataja majukumu mkubwa ya Asasi hiyo kuwa ni kushirikisha Vyombo vya Haki Jinai ambavyo ni Mahakama, Polisi, Magereza pamoja na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Nchini katika kupata namna bora ya kupunguza Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu Magerezani.
Naye Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amesema kuwa Jeshi la Magereza lipo katika Maandalizi ya kuwa na Mtaala Bora utakaowafanya Maafisa wa Jeshi hilo kuweza kukubalika Kimataifa katika Huduma za Urekebishaji.
Aidha, amesema kuwa anajivunia kuwa na ushirikiano mzuri na Maafisa Waandamizi Wastaafu wa Jeshi la Magereza katika kukamilisha jukumu la Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani.
Asasi hiyo kwa sehemu kubwa inaundwa na Maafisa Waandamizi Wastaafu wa Jeshi la Magereza wakiwemo Makamishna Wakuu ambao wamedhamilia kutoa uzoefu wao wa Uendeshaji wa Magereza wa ndani na nje kwa Serikali kupitia Vyombo vya Haki Jinai likiwemo Jeshi la Magereza.
Comments
Post a Comment