Skip to main content

Kibadeni amtimua Henry Joseph


Henry Joseph

IUNGO wa Simba, Henry Joseph, ameondolewa katika kambi ya Simba huku Ramadhan Chombo ‘Redondo’ akirudishwa kikosi cha pili.
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata, zinasema Henry ambaye amesajiliwa na Simba msimu huu huku akilipwa mshahara wa Sh1.5 milioni, alikorofishana na kocha wake, Abdallah Kibadeni, Jumatatu wiki hii katika mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika katika  Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.
Henry anayemudu kucheza nafasi ya ulinzi na kiungo, alirudi nchini mwaka huu akitokea klabu ya Kongsvinger ya Norway iliyoshuka daraja.  Kurejea kwake kumetokana na kukataa mkataba mpya wa klabu hiyo wenye pesa kiduchu baada ya timu kuyumba kiuchumi.
Jumatatu wiki hii, wakati Simba ikiwa katika mazoezi ya asubuhi kabla ya kuondoka jioni yake kwenda kambini Bamba Beach, Henry alifanya mazoezi ya kukimbia pekee yake na baadaye wachezaji wote walipofika uwanjani Kibadeni aliwataka wakimbie kwa pamoja, lakini Henry inadaiwa aligoma kwa madai kuwa alikuwa tayari ameshafanya mazoezi ya peke yake.
Hata hivyo, Henry alipozungumza na Mwanaspoti jana Jumatano, alikanusha vikali madai hayo na kusema kuwa hawezi kufanya kitendo kama hicho maishani mwake kwani anaheshimu wajibu wake.
“Sijawahi kufanya utovu wa nidhamu kwa kocha. Nilifika pale saa 11 alfajiri, nilikuwa wa kwanza. Nikafanya mazoezi ya kukimbia pekee yangu ili kujiweka fiti kwa sababu muda mwingi nilikuwa majeruhi. Baadaye wenzangu walipofika nikajumuika nao, lakini Julio (Jamhuri Kihwelu) akaniambia nipumzike kwani nimechoka,” alisema Henry.
Alisema alivyoambiwa hivyo alimfuata Kibadeni kumwambia kuwa ameambiwa na Julio apumzike na baada ya hapo akawa amekaa nje ya uwanja huku wenzake wakiendelea na mazoezi.
“Nilishangaa wakati Kibadeni anatangaza kikosi cha kuingia kambini Bamba Beach, alisema sitakwenda na timu, badala yake nikafanye mazoezi ninayoyajua mimi na kwamba akinihitaji ataniita,” alisema Henry.
Alisema anamheshimu kila mtu na kwamba katika maisha yake amejitahidi kufuata misingi na nidhamu ya soka na ndio maana bado haelewi kisa kilichotokea mpaka Kibadeni kuamua kumuacha.
Henry alisema ili kujiweka fiti, ameendelea kufanya mazoezi asubuhi na jioni na wakati mwingine amekuwa akienda gym, lakini kwa sasa hayupo katika mazoezi ya Simba.
Mwanaspoti ilimtafuta Kibadeni kuzungumzia hilo na alilisukuma suala hilo kwa Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye majibu yake hayakuwa ya moja kwa moja, lakini yalitosha kuthibitisha.
Julio alisema kila mchezaji anatakiwa kuwa na nidhamu na kujituma katika mazoezi na kwenye mechi na asiyefanya hivyo hurudishwa kikosi cha pili.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...