Bw. Shahid Yusuf ambaye ni Consultant wa AFCE akichangia hoja katika mkutano wa ujumbe wa Tanzania na Benki ya Dunia.(Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma – Washington DC)Ujumbe wa Tanzania katika mkutano na Benki ya DuniaBw. Paul Brenton Trade Practice Leader- AFTPM akitoa ufafanuzi pembeni yake ni Bw. Danny Leipziger – aliyekuwa Mkuu wa Idara ya kupunguza umasikini na kuinua uchumi.Kutoka kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe na Naibu Gavana wa BOT Bi. Natu Mwamba wakitafakari kwa makini majadiliano hayo.Bw. Zenfack, katikati akifafanua jambo katika mkutano huo, kulia ni Bw. Philippe Dongier Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi.
Ujumbe wa Tanzania wakutana na Benki ya Dunia mjini Washington DC na kufanya majadiliano juu ya usimammizi wa uchumi wa Tanzania. Akizungumza katika mahojiano hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa kikubwa kilichojadiliwa katika majadiliano hayo ni masuala ya ajira kwa vijana na wanawake.
‘Katika suala zima la ajira tumeangalia ni namna gani tunaweza kuzalisha ajira zaidi na ni sekta zipi ambazo ni muhimu, na ambazo tunaweza kuziangalia. Suala la kilimo ndio hasa limeonekana kuwa na tija zaidi kwa sababu kilimo kinachukua watu wengi sana kwa Tanzania.’ Alisema Likwelile.
Katika mazungumzo hayo ujumbe kutoka Tanzania uliweza kujadiliana na Benki ya Dunia kuhusiana na miundombinu hasa barabara, masuala mazima ya upatikanaji wa umeme pamoja na masuala ya bandari.
Katika mazungumzo hayo walijikita zaidi katika sekta zisizo rasmi ambapo ndiko kuna watu wengi na wamekubaliana kuwa wataangalia ni namna gani tija inaweza kuimarishwa na masuala mazima ya ajira, elimu na ujuzi wa watu kuweza kufanya kazi.
Katika kuhitimisha majadiliano hayo Dkt. Likwelile alisema kuwa Benki ya Dunia wanakamilisha ripoti kwa kushirikiana na tume ya mipango ili baadae tuwe na vitu ambavyo vitasaidia katika sera zetu na suala zima la ajira na uchumi mzima unaweza kuangaliwa.
Mikutano hii ya mwaka bado inaendelea hapa mjini Washington DC.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Washington D.C
Comments
Post a Comment