DRC ilisusuia shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kutokana na maandiko yake
Shughuli
ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali na
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,iliyokukuwa imepangwa kufanyika
Jumatatu , iligonga mwamba.
Hii ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.
Mpatanishi
wa pande hizo mbili Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo
hazikuwa tayari kuonana ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie
saini mkataba katika chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.
Hata
hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa hilo kufanyika kwa sababu pande
zinazozozana lazima zikae katika chumba kimoja kwa ajili ya kufanikisha
juhudi za upatanishi.
Kundi
la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada ya kupata kipigo kutoka kwa
wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa
waliowafurusha kutoka maficho yao ya milimani katika mpaka wa Rwanda na
Uganda.
Mkataba huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyewe ilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.
Mwandishi
wa BBC mjini Kampala, Ali Mutasa anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono
Opondo alisema mkataba hautatiwa saini na kwamba haijulikani ni lini
makubaliano hayo yatasainiwa. Alisema Upande wa M23 uko tayari kwa
shughuli hiyo na kuwa kizungumkuti kimetokana upande wa DRC.
Serikali
ya DRC kupitia kwa msemaji wake,Lambert Mende ilisema kuwa Kinshasa iko
tayari kutia saini makubaliano hayo, lakini sio mkataba unaosema ni
makubaliano ya amani kwa sababu ni kama kundi hilo bado lipo.
Duru
zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja na wanadiplomasia wa nchi za
Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini lakini wajumbe wa DRC
hawakuingia katika chumba cha hafla hiyo ya kutia saini.
Comments
Post a Comment