LIGI
kuu soka nchini England (EPL) imeendelea usiku huu kwa mechi moja kubwa
kupigwa baina ya washika bunduki wa London, klabu ya Asernal dhidi ya
Chelsea.
Kipute hicho kimepigwa katika dimba la Emirates na kushuhudia timu hizo zikitoka suluhu pacha ya bila kufungana (0-0).
Mchezo
wa leo ulikuwa muhimu kupata ushindi kwa kocha Aserne Wenger, kwani
amekutana zaidi ya mara 10 na Mourinho wote wakiwa makocha na kushindwa
kupata matokeo ya ushindi.
Asernal
walicheza vizuri na kufika mara kadhaa katika eneo la hatari la
Chelsea, lakini walishindwa kutikisha nyavu za wapinzani wao.
Ulikuwa usiku mzuri kwa Mourinho, kikosi chake kilicheza vizuri sana na kuonesha uimara, lakini mipango yake ilikataa.
Pia
mechi hii ilikuwa muhimu kwa Asernal kwani walitakiwa kushinda ili
kurejea kileleni mwa msimamo wa EPL baada ya Liverpool kushinda wikiendi
na kushikilia usukani kwa kujikusanyia pointi 36.
Kwa
matokeo ya suluhu, Asernal wanabakia nafasi ya pili kwa kujikusanyia
pointi 36 sawa na Liverpool, lakini wanazidiwa kwa wastani mzuri wa
mabao ya kufunga na kufungwa.
Sasa
Majogoo wa jiji wanaojivunia ubora wa Luis Suarez wanaendelea kukaa
kileleni mwa ligi kuu soka nchini England na wengine wakiisoma namba.
Shughuli inaanza: Wachezaji wa Arsenal na Chelsea wamekutana usiku huu katika mchezo mgumu dimba la Emirates
Nafasi ya tatu inakaliwa na
Manchester City wenye pointi 35, huku Chelsea wakibakia katika nafasi
yao ya nne kwa pointi 34, sawa na Everton waliopo katika nafasi ya tano,
lakini tofauti ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabingwa watetezi, Manchester United wapo nafasi ya nane na pointi zao 28 na juu yake yupo Tottenham Hospurs mwenye pointi 30.
Kikosi cha Arsenal usiku huu: Szczesny 6, Sagna 7, Mertesacker 7, Vermaelen 7, Gibbs 7, Ramsey 6, Arteta 7, Walcott 6, Ozil 6, Rosicky 6, Giroud 6.
Wachezaji wa akiba: Podolski, Monreal, Cazorla, Flamini, Fabianski, Bendtner, Jenkinson.
Kikosi cha Chelsea: Cech 6, Ivanovic 7, Cahill 7, Terry 7, Azpilicueta 7, Mikel 6, Lampard 7, Ramires 6, Willian 6, Hazard 7, Torres 6.
Wachezaji wa akiba: Cole, Luiz, Mata, Oscar, Schurrle, Schwarzer, Eto’o.

Macho kwenye mpiral: Mikel na Arteta wakichuana kwenye mpira
Amaruka juu: Fernando Torres akiruka juu kupiga kichwa mpira kwenye eneo la penati la Chelsea
Akipiga krosi: Gary Cahill akipambana na mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud
Ikigonga besela: Frank Lampard akiangalia mpira uliopiga na kugonga mwamba
Comments
Post a Comment