Majeshi ya Sudan Kusini yanajiandaa kupambana na waasi katika mji wa Bor, Rais Salva Kiir amesema.
Rais
Kiir ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba majeshi yapo tayari na
kuongeza kuwa mashambulizi yalichaleweshwa ili kuruhusu raia wa Marekani
kuondolewa katika eneo hilo.
Bor, ni eneo lililokuwa na mgogoro ambalo lipo ndani ya jimbo la Jonglei lililoangukia mikononi mwa waasi siku ya jumatano.
Takribani
wiki imepita tangu mapigano ya kikabila yaanze na kusababisha hofu kwa
raia. Maafisa ya shirika la misaada wamelielezea eneo hilo kuwa na
matukio ya umwakigaji damu pamoja na mauaji.
Mapema
Majeshi ya Sudan Kusini yamethibitisha kuwa Bentiu, mji wenye utajiri
wa mafuta katika jimbo la Unity limeangukia mikononi mwa wapiganaji
wanaoungwa mkono na Makamu wa Rais aliyestaafu Riek Machar.
Rais Kiir , kutoka kabila kubwa nchini humo la Dinka, mwezi julai alimfuta kazi Bwana Machar anatokea jamii ya Nuer.
Rais Kiir anamtuhumu Bwana Machar kwa kufanya jaribio la kumpindua, jambo linalopingwa vikali na Machar.
CHANZO: BBCSWAHILI
Comments
Post a Comment