Shilingi
bilioni 43 kati ya bilioni 50.03 za mpango wa uwezeshaji wananchi
kiuchumi na kuongeza ajira, maarufu kama “Mabilioni ya JK” zimerejeshwa
kutoka kwa wajasiriamali 74,701 waliokopeshwa na serikali kwa awamu
mbili tofauti katika mikoa yote nchini.
Fedha hizo zilitolewa kwa utaratibu wa serikali kutoa dhamana ya mikopo kwenye benki za CRDB, NMB, Community na Benki ya Posta.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, alisema hayo katika mkutano kati yake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya nne katika maeneo yanayohusu Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema wananchi waliokopeshwa fedha hizo wamepiga hatua kubwa kiuchumi na kwamba, serikali inaendelea kukusanya marejesho ya madeni ya mikopo iliyochukuliwa.
Kwa mujibu wa Waziri Nagu, hali hiyo ni uthibitisho kwamba Watanzania ni watu wanaoaminika pale wanapofuatiliwa.
Kutokana na hali hiyo, alisema serikali hivi sasa inafanya tathmini kuangalia uwezekano wa kuendelea kuwakopesha wananchi wengine ili kuwakomboa kiuchumi.
Aidha, alisema serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuhamasisha na kuvutia miradi ya uwekezaji nchini.
Alisema serikali itaendelea kuhamasisha uwekezaji nchini kwa kuboresha na kutekeleza sera na sheria zitakazovutia uwekezaji kwani inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.
Waziri Nagu alisema kutokana na jitihada za serikali za kuweka mazingira wezeshi na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, idadi na thamani ya miradi iliyoidhinishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
“Na hii inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania,” alisema Dk. Nagu.
Alisema ili kuendelea kuboresha sera na sheria za uwekezaji ziendane na mazingira na mahitaji ya uwekezaji, serikali imeshakamilisha maandalizi ya taarifa ya mapitio ya sera zinazohusu uwekezaji.
Kwa mujibu wa Waziri Nagu, maandalizi hayo yalifanyika kwa kutumia mfumo wa kutathmini sera za uwekezaji unaotumiwa na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).
Alisema nia ya serikali ni kuhakikisha sekta binafsi inachukua nafasi yake kwa kuwa ni moja ya misingi ya uchumi wa soko, hivyo akasema hakuna Mtanzania mwenye uwezo atakayekataliwa kuwekeza ili kukuza uchumi wa nchi.

CHANZO: NIPASHE
Comments
Post a Comment