Mamia
ya abiria wamekwama kusafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo
mikoani na nchi jirani cha Ubungo (UBT) jijini Dar es Salaam, kufuatia
kupanda kwa nauli na uchache wa magari uliopo hivi sasa.
Hali hiyo ilioneka jana saa 4:00
asubuhi baada ya NIPASHE kutembelelea kituo hicho na kushuhudia idadi
kubwa ya wasafiri wanaokwenda mikoani wakiwa wamekwama huku wengine
wakiamua kupiga kambi kituoni hapo wakiwa na watoto pamoja na mizigo.
Wakizungumza na NIPASHE, baadhi ya abiria waliokumbwa na adha hiyo hususani wale wanaosafiri kuelekea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Kagera na Kigoma, walisema mamlaka za udhibiti na usimamizi wa usafirishaji wa abiria zimeshindwa kazi kutokana na tatizo hilo kujitokeza kila ifikapo mwisho wa mwaka.
Walisema kuwa mbali na kuwapo kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Chama Cha Kutetea Abiria (Chakua) pamoja na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Nchini (Taboa), hakuna juhudi zinazoonekana kusaidia abiria.
“Kwa kweli wananchi tunapata shida sana na hapa Sumatra wapo humu ndani tangu asubuhi, lakini mchezo wa urushaji (kupanda) nauli upo pale pale, inafika wakati baadhi ya abiria leo wengine wamepanda magari ya mizigo ya Fuso kwa Shilingi 25,000 kwenda Tanga,” alisema Zuberi Abbas.
Walisema kuwa katika kipindi cha kawaida, nauli ya kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga ni Sh.12,000, lakini tangu jana abiria walikuwa wanatozwa nauli ya kuanzia Sh. 25,000 hadi Sh. 40,000.
Abiria wapatao 60 waliotarajia kusafiri jana kuelekea mkoani Mara kwa basi la ‘Musoma Express’ walionekana wakitoa malalamiko yao Sumatra, Polisi na kwa wakala wa basi hilo kutokana na kucheleweshwa safari yao iliyotakiwa kuanza saa 12:00 asubuhi, lakini walikuwa bado kituoni hadi kufikia saa 5:10.
Kwa upande wa usafiri wa mabasi yaendayo mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, hali ilionekana kuwa shwari licha ya nauli kupanda tofauti na iliyopangwa na Sumatra.
Mabasi ya kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa yamepandisha nauli kati ya Sh. 22,000 na 30,000 kutoka Sh.18,000.
Msemaji wa Chakua, Gervas Rutaguzinda, alithibitisha kuwapo kwa shida ya usafiri kwa abiria waendao mikoani na kusema kuwa hatua zilizochukuliwa ni kutafuta mabasi mengine ya ziada ili kuwasafirisha.
Alisema kuwa abiria zaidi ya 120 watasafirishwa na mabasi ya kampuni ya ‘Princess Muro’ kuelekea mikoa ya Kaskazini iliyojitolea kuwasafirisha kwa nauli iliyopangwa na Sumatra.
“Usafiri ni wa shida na abiria kama mnavyoona wamejaa humu ndani Ubungo, lakini kuna mabasi mawili ya kampuni hii ambayo siyo ‘route’ yao kuelekea Arusha, wamejitolea kusafirisha abiria hawa na watawatoza nauli ya siku zote,” alisema Rutaguzinda.
Naye Mjumbe wa Taboa, Mustapha Mwalongo, alisema tatizo halipo kwenye mabasi ila ni kutokana na msimu wa mwisho wa mwaka kuwa na abiria wengi kuliko wakati mwingine.
Alisema kuwa walishatoa agizo kwa abiria na mawakala wa mabasi kukata tiketi za abiria ndani ya ofisi na siyo nje ya ofisi ili kuepuka udanganyifu na usumbufu unaoweza kujitokeza.
“Mabasi yanayosafirisha abiria kila siku ni yale yale, ila abiria wameongezeka. Kipindi hiki vyuo, shule, wafanyakazi wa serikalini wanapewa likizo mwisho wa mwaka, hii inaleta msongamano mkubwa wa abiria,” alisema kisha kuongeza kuwa kungekuwa na utaratibu wa kubadili msimu wa kufunga shule ili kupunguza msongamano huo.
Alisema kwa hali ya sasa abiria anayetarajia kusafiri kesho yake hana uhakika wa safari kwa kuwa hakuna kampuni yenye mabasi mengi ya kukata tiketi siku hiyo na kuondoka.
“Kwa hapa nchini, hakuna mmiliki wa mabasi mwenye magari ya ziada, bado hatujafikia viwango vya nchi nyingine abiria anakatiwa tiketi ya safari ya kesho huku analiona gari likiwa limeegeshwa, sisi ni tofauti gari linakuwa safarini siku hiyo na lolote linaweza kujitokeza njiani kama ajali na hata kuharibika na safari ya kesho yake isiwapo,” alisema Mwalongo.
Kamanda wa Polisi UBT, Yussuf Kamotta, alisema wamedhibiti watu wanaosafirisha abiria kwa magari ya mizigo hususani Fuso na kwamba wanashirikiana na Sumatra ili kutoa vibali vya muda vya kuwasafirisha abiria ambao wamekwama kituoni hapo.
Naye Ofisa Leseni Udhibiti Sumatra, Sebastian Lehay, alisema kuwa kumekuwapo na ongezeko la abiria kila ifikapo mwisho wa mwaka na wamekuwa wakitoa ushauri kwa abiria kukata tiketi mapema.

CHANZO: NIPASHE
Comments
Post a Comment