Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli
Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa
cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa
kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya
Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili
wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na
kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa
Wilayani Mpwampwa.
Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano
ambayo hayakusombwa na maji katika ajali
iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya
Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya
Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea
Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa
yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.
Njia ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni
ya Gulwe Wilaya ya Mpwampwa kutokana na mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno
mbambali nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban
Mwinjaka akitoka kwenye maji baada ya kuangalia
kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na
maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya
Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo, kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali
za nchi. Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu
wawili na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa
katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani
Mpwampwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban
Mwinjaka akimfariji mmoja wa Majeruhi wa Ajali ya
treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe
Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika
hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Wilayani
Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya
mizigo imetokea usiku wa kuamkia leo na
kusababisha kifo cha watu wawili na wengine saba
kujeruhiwa.
Comments
Post a Comment