Mto Ruaha ni moja ya mito ambayo maji yake
kwa kiasi kikubwa sio masafi
yamechanganyikana na tope, hali hiyo
imesababisha kuwa na mazalio mengi ya
samaki aina ya Kambale, Samaki hao ambao
wanauwezo wa kuishi kwa muda mrefu hata
kama hakuna maji kutokana na kwamba huwa
na uwezo wa kujizika ndani ya tope hata kwa
miezi zaidi ya sita.
Wavuvi wa eneo hilo wamekuwa
wakijishughulisha na uvuvi wa samaki aina
mbalimbali lakini zaidi huvua samaki aina ya
Kambale, Hivi karibuni wamevua Kambale
mkubwa sana na kukili kwamba alikuwa ni
moja ya samaki wakubwa ambaye wamemvua.
Wamesema kwamba walisha wahi kuvua
samaki aina hiyo mkubwa lakini hakufikia
samaki huyo aliyevuliwa hivi karibuni.
"Ni kweli tumekuwa tukivua sana samaki lakini
huyu ni samaki mkubwa sana ambaye
tumemvu" aliongea Mvuvi.
Huyu ni Samaki Mkubwa ambaye alionekana
pembezoni mwa Mto Ruaha Iringa Mara baada
ya Kuvuliwa tayari kwa kuingizwa Sokoni.
Samaki huyo akiwa anaonekana kwa ubavuni.
Picha na Iringa yetu
Comments
Post a Comment