Skip to main content

SOMA HAPA HOTUBA YA MH.TUNDU LISSU ALIYOITOA KATIKA BUNGENI MALUMU LA KATIBA Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba Mhe. Tundu Lissu alipokuwa akitoa Hotuba ya Maoni ya walio wachache kutoka katika Kamati Na.4 kabla ya Kukatiwa matangazo na Kituo cha matangazo cha TBC MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE KUHUSU SURA ...HII NDIYO HOTUBA YA MH.TUNDU LISSU ALIYOITOA KATIKA BUNGENI MALUMU LA KATIBA

Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba Mhe. Tundu Lissu alipokuwa akitoa
Hotuba ya Maoni ya walio wachache kutoka katika Kamati Na.4 kabla ya
Kukatiwa matangazo na Kituo cha matangazo cha TBC
MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE
KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
[Kanuni ya 32(4) ya Kanuni za Bunge Maalum, 2014]
UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’) ndizo msingi ambao Rasimu yote
imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa suala la muundo wa
Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya Sita inahusu
‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo
wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya
miaka thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri
Kuu ya Chama cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa ya chama hicho imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo
moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi.”
Suala hili pia limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka
mitatu iliyopita. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Joseph Sinde Warioba wakati wa kuwasilisha Ripoti ya Tume yake kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar tarehe 30 Disemba, 2013:
“Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu Rasimu
ya awali ilipotolewa ... ni Muungano wa Tanzania. Jambo kubwa limekuwa juu
ya muundo wa Muungano.”
Umuhimu wa suala hili unathibitishwa pia na uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya
Bunge Maalum kuelekeza kwamba Kamati zake Namba Moja hadi Kumi na
Mbili zianze kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Haya ni maoni ya
wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne juu ya Sura hizi mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mjadala wa Kamati Namba Nne kuhusu Sura za Kwanza na Sita za Rasimu
unathibitisha pia umuhimu wa suala la muundo wa Muungano katika mjadala
mzima wa Rasimu. Kama Taarifa ya Kamati yetu inavyoonyesha, Kamati
Namba Nne imeshindwa kufanya uamuzi kuhusu suala hili katika ibara za 1 na
60 za Rasimu. Katika ibara ya 1 ya Sura ya Kwanza, wajumbe walio wengi
walipata kura 22, ambayo ndiyo theluthi mbili ya kura za wajumbe wote 33 wa
Tanzania Bara wa Kamati Namba Nne. Kwa upande wa Zanzibar, wajumbe
walio wengi walipata kura 9 ambayo ni pungufu ya kura 13 zinazohitajika ili
kufikisha idadi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 19 wa Zanzibar.
Kwa upande wa ibara ya 60, wajumbe walio wengi walipata kura 22 za
wajumbe kutoka Tanzania Bara, ambazo ni theluthi mbili ya idadi ya wajumbe
wote 33 kutoka Tanzania Bara. Aidha, kwa Zanzibar, wajumbe walio wengi
walipata kura 8, ambazo pia ni pungufu ya kura 13 zinazotakiwa kufikisha
idadi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 19 kutoka Zanzibar. Kwa sababu hiyo,
ibara za 1 na 60 za Rasimu hazikupitishwa au kuamuliwa na Kamati Namba
Nne kama inavyotakiwa na kifungu cha 26(2) cha Sheria na kanuni ya 64(1)
ya Kanuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sasa tunaomba kwa ridhaa yako, tuwasilishe hoja na sababu za maoni ya
wajumbe walio wachache katika Kamati Namba Nne kuhusu Sura hizi mbili
ambazo ndio ‘moyo wa Rasimu.’
SURA YA KWANZA
Sura ya Kwanza ya Rasimu inahusu ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’
Sehemu ya Kwanza ya Sura hiyo inazungumzia ‘jina, mipaka, alama, lugha na
tunu za Taifa.’ Ibara ya 1 inaitambulisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
ibara ya 2 inatangaza ‘eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’; na ibara
ya 3 inaweka utaratibu wa ‘alama na sikukuu za Taifa.’ Vile vile ibara ya 4
inaweka utaratibu wa lugha ya Taifa na lugha za alama, wakati ibara ya 5
inahusu ‘tunu za Taifa.’
Kwa upande wake, Sehemu ya Pili ya Sura ya Kwanza inaweka masharti ya
‘mamlaka ya wananchi, utii na hifadhi ya Katiba. Ibara ya 6 ya Sehemu hiyo
inatoa ufafanuzi wa ‘mamlaka ya wananchi’; ibara ya 7 inafafanua uhusiano
kati ya ‘watu na Serikali’; ibara ya 8 inashurutisha ‘ukuu na utii wa Katiba’; na
ibara ya 9 na ya mwisho inaweka ‘hifadhi ya utawala wa Katiba.’
IBARA YA 1
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kama maelezo yake ya pembeni (marginal note) yanavyoonyesha, ibara ya 1
inaitambulisha ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Ibara ya 1(1) inatamka
kwamba “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka
kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za
Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.”
Kwa upande wake, ibara ya 1(2) inafafanua kwamba Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania “ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi
vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu
haki za binadamu na lisilofungamana na dini.” Mwisho, ibara ya 1(3)
inatukumbusha kwamba “Hati ya Makubaliano ya Muungano ... ndio msingi
mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadri
itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.”
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne wanapendekeza mabadiliko
ya jina la nchi yetu kutoka jina la sasa la ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’
kuwa jina jipya la ‘Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.’ Aidha,
wajumbe hao wanapendekeza kuacha kutajwa kwa Hati ya Makubaliano ya
Muungano ya mwaka 1964 katika ibara ya 1(1) na (3) ya Rasimu. Badala yake,
inapendekezwa kwamba Katiba hii ndiyo iwe msingi wa Shirikisho la Jamhuri
za Tanganyika na Zanzibar.
Kwa mapendekezo haya, ibara ya 1(1) itasomeka kama ifuatavyo: “Shirikisho
la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar ni Shirikisho ambalo limetokana na
Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar.” Kwa mantiki hiyo, ibara ya 1(2) itasomeka: “Shirikisho la Jamhuri
za Tanganyika na Zanzibar ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa
vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria,
kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.” Aidha, ibara ya 1(3)
itasomeka: “Katiba hii ndio msingi mkuu wa Shirikisho la Jamhuri za
Tanganyika na Zanzibar.” Zifuatazo ni hoja na sababu za mapendekezo haya.
SHIRIKISHO AU MUUNGANO?
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Katika nusu karne ya uhai wake, nchi yetu imeitwa ‘Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.’ Hata hivyo, katika kipindi chote hicho, Katiba na Sheria za nchi yetu
hazijawahi kufafanua kwa uwazi aina au haiba ya ‘Muungano’ huu. Matokeo ya
kukosekana kwa ufafanuzi huu ni kwamba katika nusu karne hiyo, kumekuwa
na mjadala mkubwa wa kikatiba, kisiasa na kitaaluma kuhusu suala la kama
Jamhuri ya Muungano ni dola ya muungano (a unitary state), au ni dola ya
shirikisho (a federal state). Majibu ya swali hili yamekuwa na athari za moja
kwa utambulisho, haki, maslahi na wajibu wa Washirika wa Muungano huo,
yaani Tanganyika na Zanzibar, na hasa kwa wananchi wa nchi hizi mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kukosekana kwa ufafanuzi wa aina ya muungano wetu haujawa suala la
mijadala ya kisiasa na kikatiba peke yake, bali kumekuwa ni chanzo cha
migogoro mikubwa ya kisiasa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Migogoro hii ilianza tangu mwanzo kabisa wa
Muungano wakati wa sakata la kuwa na ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani
Magharibi kwa upande wa Tanganyika na ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani
Mashariki kwa upande wa Zanzibar.
Aidha, kati ya mwaka 1964-1967 ulizuka mgogoro mkubwa kuhusiana na
uwakilishi wa Zanzibar katika iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na
uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania; kuunganishwa kwa vyama vya ASP na
TANU na kuundwa kwa CCM mwaka 1977, na katika mjadala wa marekebisho
ya Katiba wa mwaka na baadae ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa
Zanzibar’ mwaka 1983/1984.
Baadae mwaka 1988 ulitokea mgogoro mkubwa uliopelekea kung’olewa
madarakani kwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim
Seif Shariff Hamad na baadae kufukuzwa katika CCM; wakati wa harakati za
kudai kura ya maoni kuhusiana na Muungano mwaka 1989/1990; wakati wa
mjadala wa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1991;
wakati wa sakata la Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu
(Organization of Islamic Countries - OIC) mwaka 1993; wakati wa mjadala wa
G-55 na madai ya kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano
mwaka 1994, na Uchaguzi Mkuu wa 1995 huko Zanzibar.
Milenia Mpya ilipoanza ilianza na mgogoro kuhusu matokeo ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2000 uliopelekea mauaji ya Januari 2001 huko Zanzibar.
Mgogoro huo ulifuatiwa na mgogoro juu ya suala la ugunduzi wa mafuta
visiwani Zanzibar; harakati za kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki
na hivi karibuni kupitishwa kwa Marekebisho ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar
ya 1984 mwaka 2010.
Zaidi ya migogoro hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi
zanzibar zimeunda tume na kamati nyingi ili kupata dawa ya ‘Kero za
Muungano.’ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar peke yake imeunda tume na
kamati 13 katika kipindi kifupi cha miaka 12 kuanzia mwaka 1992 hadi 2004;
wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeunda tume na kamati nane
kushughulikia matatizo hayo. Licha ya jitihada zote hizo, ‘Kero za Muungano’
hazijapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tangu miaka ya mwanzo ya Jamhuri ya Muungano kulikuwa na mitazamo
miwili tofauti miongoni mwa waasisi na viongozi wakuu wa Jamhuri ya
Muungano. Mitazamo hii tofauti inathibitishwa na kauli ya Mwalimu Julius K.
Nyerere, mwasisi na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano katika
Mkutano Maalum wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika Dodoma kati ya
tarehe 24-30 Januari, 1984: “... Muungano wa Tanzania ukiangalia kwa jicho la
Zanzibar ni wa shirikisho lakini ukiangalia kutoka upande wa Tanzania Bara ni
Serikali moja.”
Mwalimu alikuwa akimjibu Makamu Mwenyekiti wa CCM, Makamu wa Rais na
Rais wa Zanzibar wakati huo, Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi aliyesema kwamba
Muungano wa Tanzania umeunda Shirikisho (Federation) na sio Serikali moja
(Unitary State). Mjadala huo ulipelekea ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya
kisiasa Zanzibar’ na kung’olewa madarakani kwa Jumbe, Waziri Kiongozi
wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Kwaw Swanzy.
Aidha, Wolfgang Dourado, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati
Hati ya Muungano inasainiwa, na mkosoaji mkubwa wa Muungano huo,
aliwekwa kizuizini kwa kuunga mkono hoja za Rais Aboud Jumbe.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Miaka kumi baada ya ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar’
Jamhuri ya Muungano ilikabiliwa na mgogoro mwingine tena wa kikatiba na
kisiasa, mara hii ukitokana na Zanzibar kujiunga na OIC. Kitendo hicho kilizua
tafrani kubwa ya kisiasa pale Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipopitisha
Azimio la kutaka kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano
mwezi Agosti, 1993. Azimio hilo liliungwa mkono na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, kitendo kilichomfanya Mwalimu Nyerere kuingilia kati na kuzima
jaribio hilo.
Baadae Mwalimu aliandika kitabu alichokiita Uongozi Wetu na Hatima ya
Tanzania kilichochapishwa mwaka 1994. Katika kitabu chake, Mwalimu
anarejea mkanganyiko ambao umekuwepo kuhusu aina ya Muungano huu kwa
maneno yafuatayo:
“Nchi zinapoungana na kuwa nchi moja mifumo ya kawaida ya miundo ya
Katiba ni miwili: Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafuta serikali yake, na nchi
mpya inayozaliwa itakuwa ni nchi moja yenye serikali moja. Katika mfumo wa
pili kila nchi itajivua madaraka fulani ambayo yatashikwa na serikali ya
shirikisho, na itakuwa na serikali ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo
yaliyobaki. Mambo yatakayoshikwa na serikali ya shirikisho ni yale ambayo
yakibaki katika mamlaka ya nchi zilizoungana, basi kwa kweli nchi hizo
zitakuwa hazikuungana kuwa nchi moja, bali zinaendelea kuwa nchi mbili
zenye ushirikiano mkubwa katika mambo fulani fulani.... Shirikisho halisi la
nchi mbili litakuwa ni nchi moja yenye serikali tatu, Serikali ya shirikisho na
serikali mbili za zile nchi mbili za awali zilizoungana kuzaa nchi mpya moja.”
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mwaka ambao Mwalimu Nyerere alichapisha Uongozi Wetu na Hatima ya
Tanzania, Makamu Mwenyekiti wake wa CCM na Makamu Rais wake hadi
Januari 1984, Alhaj Aboud Jumbe, aliyekuwa pia Waziri wa Afya wa Zanzibar
wakati Muungano unazaliwa na baadae Rais wa Pili wa Zanzibar, naye
alichapisha The Partnership: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30
ya Dhoruba. Katika kitabu hicho, Alhaj Jumbe anathibitisha kwamba “Ibara za
Mkataba wa Muungano ziliweka bayana mfumo ambao serikali kuu na serikali
shiriki katika Muungano kuwa na nguvu zinazoendeana, yaani, mfumo wa
shirikisho ambao kuna mgawiko wa mahakama, baraza la kutunga sheria na
urais baina ya serikali kuu na serikali mbili au zaidi, na kila serikali ikiwa na
nguvu kamili ndani ya mamlaka yake.”
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Aina ya dola iliyotokana na Hati ya Makubaliano ya Muungano
haikuwahangaisha waasisi wa Muungano ama viongozi wake wakuu peke
yao. Hata ndani ya makorido ya mamlaka, mjadala juu ya suala hili umekuwa
mkubwa na umeundiwa Tume na Kamati mbali mbali za kulichunguza. Kwa
mfano, hata kabla ya kuchapishwa kwa Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania
na The Partner-ship, tarehe 6 Aprili, 1992, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Salmin Amour aliunda Kamati ya Baraza la
Mapinduzi ya Kujenga Hoja Juu ya Masuala ya Muungano wa Tanzania,
maarufu kama Kamati ya Amina Salum Ali kutokana na jina la Mwenyekiti
wake. Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna, ambaye ni mjumbe wa Bunge hili
Maalum, alikuwa Katibu wa Kamati hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Kamati ya Amina Salum Ali ililichunguza suala la
aina ya Muungano uliozaliwa na Hati ya Makubaliano ya Muungano. Jibu la
Kamati hiyo lilikubaliana na nusu ya hoja ya Mwalimu Nyerere na nusu ya hoja
ya Alhaj Aboud Jumbe: “... Muungano wa Tanzania, haidhuru unaitwa ‘Union’,
lakini uko kati na kati baina ya ‘Union’ na Shirikisho. Kuwepo kwa Serikali ya
Muungano yenye madaraka makubwa ni kielelezo cha sura ya ‘Union’. Sura hii
inazidi kutiliwa nguvu na kile kitendo cha Tanganyika kuvua madaraka yake
yote na kuyaingiza katika Serikali ya Muungano. Kwa upande mwengine
kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye madaraka kamili
Zanzibar juu ya mambo yote yasiyokuwa ya Muungano, ni kielelezo dhahiri
cha sura ya Shirikisho. Kwa hivyo, Muungano huu ni wa aina yake.”
MTAZAMO WA KITAALUMA
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Hati ya Makubaliano ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar imejadiliwa sana na kwa miaka mingi katika ulingo wa
kitaaluma. Mjadala huu umehusu, kwa kiasi kikubwa, aina na muundo wa
Muungano huu. Katika kitabu chake Tanzania: The Legal Foundations of the
Union, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwezi Januari, 1990, Profesa
Issa Shivji alisema, baada ya uchambuzi wa kina wa Hati ya Muungano,
kwamba Makubaliano ya Muungano yalitengeneza katiba ya shirikisho. Kwa
mujibu wa Profesa Shivji, katiba za shirikisho zina sifa kuu zifuatazo ambazo
alisema zipo katika Hati ya Muungano:
a. Kuna mgawanyo wa wazi wa madaraka kati ya serikali kuu na serikali za
sehemu za muungano ambayo yapo katika ngazi moja; b. Mamlaka ya serikali
kuu yaliyowekewa mipaka ya wazi wakati mamlaka yaliyobaki yako mikononi
mwa serikali za sehemu za muungano; c. Serikali zote, yaani serikali kuu na
serikali za sehemu za muungano zinagusa maisha ya wananchi wao moja kwa
moja tofauti na serikali ya mkataba (confederation) ambako serikali za
sehemu ndizo zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kwa maneno
ya Profesa Shivji, kwa kuyaangalia Makubaliano ya Muungano kutoka upande
wa Zanzibar na Tanganyika na kwa ujumla wao, “... msingi wa shirikisho ndio
wenye nguvu na Makubaliano ya Muungano yanaweza kutafsiriwa kwa usahihi
kama katiba ya shirikisho.” Kwingineko katika kitabu hicho, Profesa Shivji
alidai kwamba: “Kwa vyovyote vile, ni wazi kwamba Makubaliano ya
Muungano sio katiba ya muungano (unitary constitution).”
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Msimamo wa Profesa Shivji kuhusu Makubaliano ya Muungano kuwa ni katiba
ya shirikisho umeshikiliwa kwa miaka mingi na wasomi wengine wa Muungano
huu. Hivyo, kwa mfano, katika kitabu chao cha Tanzania Treaty Practice
kilichochapishwa mwaka 1973, Earl E. Seaton na S.T. Maliti walikubali
kwamba Makubaliano ya Muungano yaliunda katiba ya shirikisho na sio katiba
ya muungano.
Miaka kumi baadae, Wolfgang Dourado, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar wakati Hati ya Muungano inasainiwa, naye alidai kwamba
Makubaliano ya Muungano hayakutengeneza dola la muungano bali
yalitengeneza ‘shirikisho la kweli.’ Wasomi wengine ambao wameitaja Katiba
ya Tanzania kama katiba ya shirikisho na wala sio ya muungano ni Profesa
B.P. Srivastava katika makala yake ya mwaka 1984 ‘The Constitution of the
United Republic of Tanzania 1977: Some Salient Features, Some Riddles’, na
Profesa Palamagamba J.A.M. Kabudi, katika International Law Examination of
the Union of Tanganyika and Zanzibar: A Federal or Unitary State?, ambayo ni
matokeo ya utafiti aliouwasilisha mwaka 1986 kwa ajili ya Shahada yake ya
Uzamili ya Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 2009 The Legal Foundations of the Union kilichapishwa kwa mara ya
pili, mara hii kikiwa na Utangulizi wa Profesa Yash Ghai, Mkuu wa Kitivo cha
Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wa kwanza kutoka Afrika
Mashariki na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Kenya iliyozaa
Katiba Mpya ya Kenya ya mwaka 2010.
Kwenye Utangulizi wake Profesa Ghai anasema kwamba licha ya Tanzania
kutokuwepo katika orodha za mashirikisho zilizoandaliwa na wasomi au na
Jukwaa la Kimataifa la Mashirikisho (International Forum of Federations); na
licha ya Katiba ya Tanzania kutokutumia neno ‘shirikisho’, bado Tanzania ni
shirikisho.
“Tanzania inakidhi vigezo vingi vya rasmi vya shirikisho: mahusiano kati ya
sehemu zake tofauti yamewekwa katika katiba, ambayo ni sheria kuu, na
hayawezi kubadilishwa katika ushirikisho wao bila kuungwa mkono na idadi
mahsusi ya wabunge wa kutoka Zanzibar na Bara ... wakipiga kura tofauti
tofauti. Katiba inaweza kufanyiwa marejeo na mahakama. Kuna aina mbili za
serikali (serikali kuu na serikali za sehemu za shirikisho), kila moja ikiwa na
mamlaka yaliyoainishwa wazi. Kuna mabunge ya shirikisho na ya sehemu
yake ... na sheria za shirikisho na za sehemu yake zikitumika katika nchi.”
MTAZAMO WA TUME
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba (‘Tume’) imetoa maelezo marefu kuhusu
madhumuni, lengo na sababu za mapendekezo ya ibara ya 1 ya Rasimu.
Pamoja na mengine, kwa mujibu wa Tume, “... lengo la ibara hii ni kuainisha
aina na hadhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni Muungano wa
Shirikisho lenye Mamlaka Kamili (Sovereign Federal State). Hatua hii ina lengo
la kuimarisha Muungano kwa kuipa Mamlaka ya Kidola Jamhuri ya Muungano
na kubainisha utambulisho, uwezo na mamlaka ya Nchi Washirika katika
Muungano.”
Malengo mengine ambayo Tume imeyataja malengo mengine kuwa ni “...
kuainisha mfumo wa utawala wa Jamhuri ya Muungano na kupanua misingi
muhimu ya nchi ...”; na kuonyesha kuwa “Hati ya Muungano ya 1964 ndio
chimbuko la Muungano wa Tanzania ... na ... kuipa hadhi ya kikatiba Hati
hiyo ... kwa ... (kuiingiza) ndani ya Katiba kama ibara inayosimama yenyewe.”
Tume imetaja sababu za mapendekezo haya kuwa ni kutekeleza matakwa ya
kifungu cha 9(2)(a) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83,
yaliyoitaka Tume “... kuongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii
ya kuhifadhi na kudumisha kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano.” Aidha, kwa
mujibu wa Tume, mapendekezo haya yatahifadhi asili, taswira na hadhi ya
Jamhuri ya Muungano katika jumuiya ya kimataifa kama inavyotakiwa na
Mkataba wa Montevideo Kuhusu Haki na Wajibu wa Nchi wa mwaka 1933,
ambao unatambua nchi yenye muundo wa shirikisho kuwa ni dola katika
sheria za kimataifa.
Tume imetambua ukweli wa kihistoria kwamba kumekuwepo mjadala wa
miaka mingi miongoni mwa Watanzania “kuhusu aina ya Muungano uliopo
Tanzania iwapo ni shirikisho au la.” Kwa sababu hiyo, pendekezo hili litaondoa
“utata wa aina na muundo wa Muungano ambao umesababisha kuvunjwa kwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Serikali zote mbili mara kadhaa.”
Tume iliridhika kwamba Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho. Kwa maneno
yake: “Shirikisho hili linatokana na muungano wa hiari wa Tanganyika na
Zanzibar ambazo zilikuwa Jamhuri zenye mamlaka kamili kabla ya kuungana
tarehe 26 Aprili 1964.” Tume inafafanua kwamba, kwa kawaida nchi ambazo
zimeingia katika muungano zinaweza kuchukua moja kati ya sura tatu:
i. Muungano wa Serikali Moja (Unitary State); ii. Muungano wa Shirikisho
(Federation); na iii. Muungano wa Mkataba (Confederation). Kwa mujibu wa
Tume, “... mfumo wa shirikisho unakuwepo pale ambapo nchi mbili au zaidi
zimeungana na hazikuunda serikali moja. Kwa maana hiyo shirikisho ...
linamaanisha mfumo wa utawala wa nchi wenye sifa zifuatazo:
1. Kunakuwa na ngazi mbili za serikali zonazotawala eneo moja la nchi na raia
wale wale; moja ikisimamia mambo ya muungano (shirikisho) na nyingine
mambo yasiyo ya muungano (yasiyo ya shirikisho); 2. Kila ngazi ya serikali,
yaani ile ya shirikisho na ile ya nchi washirika inakuwa na mamlaka kamili na
maeneo ya utendaji na uhakikisho wa kikatiba wa uhuru wa kutoingiliana baina
ya serikali hizo katika maeneo waliyo na madaraka nayo bila ya
kushauriana....; 3. Katika muundo huu, serikali ya muungano ndiyo yenye
mamlaka juu ya masuala yote yaliyokubaliwa kuwa ya muungano (shirikisho).
Serikali za nchi washirika zinakuwa na mamlaka ya kikatiba ya kushughulikia
mambo yasiyo ya muungano katika maeneo yao ya utawala; na 4. Katika
muungano wa shirikisho mamlaka kuu ya kidola (sovereign powers and
functions) yapo chini ya serikali ya shirikisho (muungano).” Mheshimiwa
Mwenyekiti,
Pamoja na kushindwa kufikisha idadi ya kura inayotakiwa na kifungu cha
26(2) cha Sheria na kanuni ya 64(1), Wajumbe walio wengi – karibu wote
wanachama wa CCM – wamependekeza kufutwa kwa ibara ya 1(1) na (2) ya
Rasimu. Badala yake, wajumbe hao wanapendekeza ibara mpya ya 1(1)
isomeke kama ifuatavyo: “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi yenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya Hati ya
Makubaliano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.”
Tofauti pekee ya mapendekezo haya na mapendekezo ya ibara ya 1(1) ya
Rasimu ni neno ‘Shirikisho.’ Hii ina maana kwamba, licha ya ushahidi mkubwa
wa kitaalamu tuliouonyesha hapa, wajumbe walio wengi wa Kamati Namba
Nne wanaamini kwamba Jamhuri ya Muungano sio Shirikisho. Kwa
mapendekezo haya, wajumbe na wanachama hawa wa CCM wanapendekeza
kuendeleza status quo, yaani sintofahamu ya kama Muungano huu
ulitengeneza dola ya ki-Shirikisho au dola ya ki-Muungano, ambayo
imeugubika Muungano kwa nusu karne ya uhai wake. Mapendekezo haya
yataendeleza pia migogoro ya kikatiba na ya kisiasa ambayo imekuwa ni
sehemu ya uhai wa Muungano huu katika kipindi hicho hadi kubatizwa jina la
‘Kero za Muungano.’Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kwa kuzingatia uchambuzi huu, ni wazi kwamba kuendelea kutumia jina la
‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ kunaendeleza hisia potofu kwamba
Makubaliano ya Muungano yalianzisha dola ya muungano (unitary state) na
sio dola ya shirikisho (federal state). Aidha, kufanya hivyo ni kuendeleza
migogoro ya kisiasa na ya kikatiba ambayo, kama tulivyoonesha, imetokana
na kukosekana kwa ufafanuzi juu ya aina ya muungano uliotokana na Hati ya
Makubaliano ya Muungano. Hii, kwa maoni yetu, haiwezi kuwa dawa ya
matatizo ya Muungano huu.
Kwa sababu hiyo, ili kuweka wazi aina ya muungano uliozaliwa na Hati ya
Makubaliano ya Muungano; ili kuondoa hisia potofu kwamba Makubaliano hayo
yalizaa dola ya muungano, ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa ‘Kero za
Muungano’, tunapendekeza kwamba maneno ‘Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania’ yaliyoko katika ibara ya 1 na ya 2 na katika ibara nyingine zote za
Rasimu yafutwe, na badala yake maneno ‘Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika
na Zanzibar’ yaingizwe katika ibara husika.
Mapendekezo yetu yana manufaa makubwa yafuatayo. Kwanza, yanaweka
wazi kwamba muungano huu ni wa dola ya ki-Shirikisho na wala sio dola ya
ki-Muungano. Pili, mapendekezo haya yanaweka bayana ukweli kwamba ni
nchi mbili huru, yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
ndizo zilizoungana. Uzoefu wa nchi nyingine zilizoungana unaonyesha
kwamba jina la muungano huweka bayana kwamba zilizoungana ni nchi zaidi
ya moja. Mifano ya wazi ya jambo hili ni majina ya Marekani (United States of
America); Uingereza (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland),
na Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates). Aidha, Urusi ya zamani
ilijulikana kama (Union of Soviet Socialist Republics) na Yugoslavia ya zamani
ilikuwa inaitwa Federal Socialist Republics of Yugoslavi

Comments

Popular posts from this blog

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HAYA NDO MANENO YA KUMPANDISHA hisia MPENZI WAKO UMPENDAE!!!!!

                                       Inawezekana wengi wetu tukawa tunayatumia bila kujua kwamba tumekusidia kuyatumia. Haya ni maneno au kauli ambazo mume/mke anaweza mwambia mwenza wake kama ishara ya kumpandisha "nyege" kabla ya kuanza  kufanya mapenzi. Wawili hawa wanaweza wakawa sehemu tofauti tofauti, mfano mume yupo kazini lakini anakaribia kurudi nyumbani, mke ukaanza "kumcharura" mumeo kwa kauli mbali mbali aidha kupitia sms au kwa kumpigia simu, ingawa kupitia sms ndo inasisimua zaidi! Hapa najua naongea na watu wazima, sina haja ya kuandika zaidi maneno yenyewe lakini kila mmoja ni mjuzi wa tabia na vitu ambavyo mwenza wake anavihusudu hasa mkiwa kitandani, mfano" Baby ukirudi leo nataka unipindishe pale katika dressing table kama ulivyonifanyia jana, na leo nimevaa lile gauni ulipendalo na zile bikini mpya, dont be late my love" Maneno haya kwa anayejua mapenzi na anampenda mkewe ni lazima huko alipo "Jogoo" awike kidog

HUYU NDIYE ALIIYELAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI NA MBWA PAMOJA NA FARASI KWA AJILI YA PESA.

When the Internet first came to the continent of  African society,most people were  very pleased with it because it reduces stress of communication with love around the world,it also serve as productive purposes like communication.It served many people for chatting, sending mails and even business. As the time passed by many ladies discovered that they could use the internet to find a chat friend or a life partner.Some girls have greatly benefited just by using the internet to find their dream marriages or relationhsips. Others have fallen into traps in the West and wish they would never have known what the internet was.This is the case of one Cameroonian,Elvire Axelle Tchamakoua. Continue....... SEE HOW IT ALL HAPPEN.... Axelle is pr00stit-te who is pimped to various men by her main man Jean Claude(French Businessman).She did not mind serving her customers from the front or from behind.The use of condoms during her encouters was the allowed as it b