Katibu Mkuu Kinana katika ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa wa
Dodoma, Kinana ataendelea na ziara kesho
katika wilaya ya Kondoa Kabla ya kuendelea katika mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHEMBA-DODOMA) Umati
wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo ukimsikiliza Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa
akizungumza na wananchi hao na kuwaasa kujitokeza kwa wingi
kijiandikisha ili kupata nafasi ya kushiriki katika upigaji kura ya
maoni Katiba inayopendekezwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Itolwa. Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuzungumza na wananchi. Nape Nnauye akiwaeleza ukweli umati wa wananchi wakuojitokeza kwa wingi katika uwanja wa Itolwa wilayani Chemba mkoa wa Dodoma. Naibu
Waziri wa Wiazara ya Habari, Vijana. Utamaduni na Michezo Mh. Juma
Nkamia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuongea na
wananchi. Mkuu wa wilaya ya Chemba Mh. Ramadhan Maneno akijitambulishwa kwa wananchi. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupiga misumari
katika paa la jengo la ofisi ya serikali ya kijiji cha Babayu. Akina mama wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika kijiji cha Itolwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakielekea eneo la mkutano katika kijiji cha Itolwa. Umati wa wananchi wakielekea katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenyekijiji cha Itolwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa chini kwenye kigoda wakati akipakwa na kuvishwa mgorole kama ishara ya heshima ya wazee wa Chemba. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Galawa kushoto na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dodoma Mh. Adam Kimbisa wakipiga plasta katika ukuta wa josho
linalokarabatiwa katika kijiji cha Gwandi. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akijitambulisha kwa wananchi katika kijiji cha Gwandi wilayani Chemba. Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akimtambulisha kwa wananchi
kijana mmoja jina lake halikupatikana mara moja akiwa amevalia kofia ya
Chadema katika kijiji cha Gwandi wilayani Chemba kijana huyo
alizawadiwa shilimgi elfu 20,000. Wananchi
wa kijiji cha Gwandi wilayani Chemba wakishiriki katika ukarabati wa
josho ambalo lilijengwa mwaka 1969 na Mwalimu J.K Nyerere Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kazi ya kujenga makenchi tayari kwa kupaua ofisi ya kata Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Galawa akijitambulisha kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Itolwa.
Comments
Post a Comment