MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA KIMATAIFA WA “LUGINA AFRICAN MIDWIVES RESEARCH NETWORK
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana
na Kaimu Muuguzi Mkuu wa serikali Dkt. Amalberga Kasangala mara baada ya
kuwasili kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach kufungua rasmi “The Scientific
Conference for Lugina Africa Midwives Research Network-LAMRN” tarehe
11.3.2015. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Ndugu Paul Makonda,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akifuatiwa na Mwakilishi kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akifungua rasmi mkutano wa kwanza wa “Lugina Africa Midwives Research
Network” uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach hapa Dr es Salaam
tarehe 11.3.2015.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria
mkutano wa Kwanza wa “Lugina Africa Midwives Research Network”
wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye
mkutano huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi kwenye meza kuu
wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akikabidhi tuzo Maalum kwa Bwana Maximillan Lugina, iliyotolewa na
wajumbe wa mkutano wa “Lugina Africa Midwives Research Network” kwa
ajili ya kumuenzi muasisi wa mtandao huo marehemu Profesa Helen Lugina
ambaye ni mkewe. Profesa Helen alikuwa ni Muuguzi kutoka Tanzania
aliyeasisi mkutano wa kwanza wa mtandao huo hapa nchini mwaka 1992.
Wawakilishi mbalimbali kutoka nchi
za Africa wanaohudhuria mkutano wa kwanza wa “Lugina Africa Midwives
Research Network” wakimzawadia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mgolole
mara baada ya kufungua rasmi mkutano huo huko Kunduchi Beach Hotel
tarehe 11.3.2015.
Comments
Post a Comment