Skip to main content

Kiama cha Wafanyakazi Waliosafiri Nje Ya Nchi chaja


Adhabu inawanyemelea watumishi wa serikali waliokaidi agizo la kutosafiri nje ya nchi bila kibali cha Rais John Magufuli na .................Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Habari zilizopatikana kutoka baadhi ya wizara  zilieleza jana kuwa tayari baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara wameshapewa orodha ya majina ya watumishi waliosafiri nje ya nchi kinyemela.

Chanzo kimoja cha habari kimesema  kuwa tayari majina hayo yamepatikana na kinachofanyika sasa ni kupitia taratibu, sheria na kanuni kabla ya kuwachukulia hatua.

Watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wamesimamishwa kazi kwa kwenda nje ya nchi licha ya maombi yao ya kusafiri kukataliwa na mamlaka.

Jana   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Donald Mmbando  alikiri kukabidhiwa taarifa kuhusu watumishi waliosafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu na kwamba kwa sasa kuna taratibu ambazo zinafanyiwa kazi na ngazi husika kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

“Ni kweli niliagiza nipatiwe taarifa ya watumishi hao na nimeshapewa ila kuna tataribu ambazo zinafanyiwa kazi na zitakapokamilika itatolewa taarifa ya wale wote waliosafiri na wamefanywa nini,” alisema Dk. Mmbando.

“Kwa sasa siwezi kulizungumzia ila likikamilika tutawajulisha.” Hivi karibuni Dk. Mmbando alitoa taarifa kwa wakuu wa Idara wizarani kwake akiwataka ifikapo Desemba 21 awe amepata taarifa ya wale wote waliokiuka agizo la Rais la kutosafiri nje ya nchi.

Dk. Mmbando aliandika dokezo kwenda kwa wakuu wa idara hiyo ambayo iliwataka kuwataja watumishi walio chini yao ambao walisafiri nje ya nchi baada ya katazo la Rais Dk. Magufuli.

Katika dokezo hilo walitakiwa kueleza watumishi hao wamesafiri kuelekea nchi gani, tarehe ya safari, madhumuni ya safari hizo, safari hizo zimegharamiwa na nani pamoja na kiasi cha fedha kilichotumika.

Waliosimamishwa kazi Takukuru ni Msemaji Doreen Kapwani, Mary Mosha, Ekwabi Mujungu na Rukia Nikitas. 

Awali, Ofisi ya Rais ilisambaza mwongozo kwa taasisi na mashirika ya umma unaoweka masharti ya ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kuyatimiza ili wapewe kibali cha kusafiri.

Masharti hayo ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi Sefue na maombi hayo yawasilishwe kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda kwa Sefue ili mwombaji aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wa safari hiyo na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.

Masharti hayo yanamtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika ama taasisi apime aone kama safari hiyo ni muhimu  kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi kabla ya kuwasilishwa Hazina.

Sharti lingine ni umuhimu wa safari hiyo na isipofanyika itaathiri vipi taifa na mwombaji  aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisi na taifa kama imewahi kufanyika huko nyuma.

Ofisi za Umma zilipokea barua kutoka kwa Msajili wa Hazina Novemba 12 mwaka huu ikieleza kuwa Rais Magufuli ametoa zuio la jumla kwa safari za nje ya nchi katika utumishi wote wa umma na mihimili yake. Barua hiyo ya Hazina ilisema zuio hilo litadumu hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...