Skip to main content

Profesa Muhongo Azidi Kuibana TANESCO


Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limeagizwa kuhakikisha hadi kufikia tarehe 3 Januari 2016 liwe................... limekamilisha kufunga umeme kwenye Jengo la Ofisi za Serikali la Mpakani  mwa Tanzania na Rwanda (One Stop Border post) lililopo eneo la Rusumo wilayani Ngara.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara kwenye Mpaka wa Tanzania na Rwanda kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Rusumo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha cha Rusumo, Laurent Gabriel alisema umeme kwenye jengo hilo umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma kwenye Ofisi zilizopo katika jengo hilo.

Gabriel aliendelea kueleza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya kukatika mara kwa mara kwa umeme na pia kukosekana kwa huduma ya mtandao wa kununua umeme kutoka nchini Rwanda.

Aidha, Profesa Muhongo alizungumza na wananchi wanaoishi maeneo ya mpakani hapo na walimueleza kusikitishwa kwao kuona jengo hilo linatumia umeme kutoka nchi jirani ambao hata hivyo walisema umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kusababisha shughuli nyingi za Serikali kukwama.

Baada ya kuelezwa taarifa hiyo, Profesa Muhongo alisema jambo hilo halikubaliki kwani tayari umeme wa Tanesco umefika kwenye eneo hilo hivyo aliiagiza TANESCO kuharakisha uunganishaji wa huduma ya umeme kwenye jengo hilo.

“Haileti maana kutumia umeme kutoka nchini Rwanda wakati Tanesco wanao umeme ambao tayari umefika mpakani hapa. TANESCO hakikisheni kufikia Jumapili ijayo (tarehe 3 Januari, 2016) jengo hili liwe limeunganishwa na umeme,” aliagiza.

Waziri Muhongo alimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Honorata Chitanda kufuatilia suala hilo kwa ukaribu ili kufikia tarehe hiyo umeme uwe umefungwa kwenye jengo hilo.

Ziara hiyo ya Profesa Muhongo ni muendelezo wa ziara za kugagua mitambo na miundombinu ya umeme nchini ambapo kwa sasa yupo Mkoani Kagera na huku akiwa amekamilisha kutembelea miradi ya umeme iliyopo maeneo ya Mikoa ya Kusini, Kaskazini, Kati na Kanda ya Ziwa.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...