Skip to main content

Profesa Ndalichako Atoa Siku 30 Kwa Katibu Mtendaji NACTE Kuvichunguza Vyuo Vyote Nchini Kujua Ubora Wake



Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa siku 30 kwa ............Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), Dk Primus Nkwera kufanya ukaguzi wa vyuo vyote na kumkabidhi ripoti ili kujiridhisha na ubora wa elimu inayotolewa.

Pia, amewataka watendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuandaa mitalaa yenye matokeo ya kujenga wanafunzi watakaozalisha kwenye jamii.

Waziri huyo ambaye amewahi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), alitoa maagizo hayo jana wakati wa ziara yake katika ofisi hizo ikiwa ni siku tano baada ya kuapishwa kuiongoza wizara hiyo.

Alisema anawafahamu vyema watendaji wote wa taasisi hizo na hatavumilia kuona ubora wa elimu ukiendelea kuporomoka nchini.

Aliitaka TET kuhakikisha mtalaa wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu) kwa darasa la kwanza na la pili unapelekwa shuleni kabla ya Januari 13.

“Lakini pili, ningependa muanze kutumia walimu wastaafu kwenye uandaaji mitalaa hiyo na ukaguzi uimarike kwa wanafunzi, mnaweza kuwa na mitalaa mizuri lakini ufuatiliaji ukikosekana haitasaidia,” alisema.

Kuhusu ubora wa elimu alisema: “Ningependa uonekane kwa matokeo baada ya kumaliza shule, sihitaji kusikia amefaulu kwa alama ngapi ila amejengewa uwezo gani kichwani,” alisema.

Alisema kasi ya uwajibikaji TET imekuwa ndogo kwani kitabu cha kurasa 16 kinatengenezwa kwa mwaka mmoja. 

“Ninaweza kuja hapa mnipatie nafasi halafu tujipime na nyie tuone, naomba mbadilike nimeona mko nyuma sana ya kasi yangu,” alisema.

Mbali na maagizo hayo, Profesa Ndalichako aliiagiza Nacte kufanya usajili wa vyuo kwa kuzingatia mahitaji ya soko badala ya kusajili holela bila ufuatiliaji kwa kuwa baadhi vinajiendesha kwa ujanja ujanja.

Alisema suala la ubora wa elimu linamkosesha usingizi. Alilitaka baraza hilo kungeongeza kasi ya ushawishi katika uwekezaji wa shule za ufundi badala ya kujikita kwenye upandishaji wa hadhi ya vyuo na kuondoa dhana ya biashara katika sekta ya elimu.

“Lakini pia ningependa wafanyakazi wote mbadilike, tuache kufanya kazi kwa mazoea. Katika upandishaji hadhi ya vyuo, lazima tujiridhishe na mahitaji ya Taifa, pia kwa suala la udahili wa wanafunzi, ningependa vyuo ambavyo havijatambuliwa kwenye mfumo wa Necta viingizwe ili kuondoa udanganyifu wa vyeti wa usajili,” alisema.  

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below: