Bajeti ya Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar Yatengwa.......Kinachosubiriwa ni ZEC Kutangaza Tarehe Ya Uchaguzi
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema bajeti ya uchaguzi wa marudio imeshatengwa na wanachosubiri ni
Mwenyekiti wa Tume ya Uhaguzi Zanzibar (ZEC) atangaze tarehe hiyo ya kufanya uchaguzi.
Amesema bajeti hiyo haitatofautiana na ile iliyotumika katika uchaguzi wa Novemba 2015 iliyofikia karibu ya shilingi bilioni saba.
Amekanusha kauli kuwa uchaguzi huo hautafanyika kwa vile matokeo yanayolazimisha kutangazwa na CUF yameshafutwa kwa mujibu wa sheria kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi, Balozi Seif amesema mazungumzo yanayoendelea ni ya kuhakiksha amani inaimarika Zanzibar na si suala la uchaguzi uliofutwa.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya miaka 52 sherehe za Mapinduzi Balozi Seif amewabeza wanaosusuia sherehe hizo kwa madia kuwa Rais Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuwa si halali ni upotoshwaji mkubwa.
Amefahamisha kuwa rais huyo yupo kihalali na hata mawaziri wake wote na watamaliza ukomo wao atakapoapishwa rais mwingine kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 28 (1) a cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na si kama inavyeleezewa kuwa ukomo wake umeisha tangu tarehe 2 Novemba.
Tazama video hii kumsikia akiongea na kujibu maswali ya waandishi kuhusu marudio ya uchaguzi Zanzibar.
Comments
Post a Comment