Skip to main content

CCM Kuwashitaki Wakuu wa Shule 15 Kwa Ubadhirifu wa Fedha


JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakusudia kuwafikisha wakuu wa shule zake 15 kwenye vyombo vya sheria kutokana na madai ya ubadhirifu wa fedha.

Akizungumza jana jijini Dar es SaIaam, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema zaidi ya shule 26 walizozifanyia ukaguzi, 15 zimekutwa zikiwa na upungufu na kubwa ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa fedha.

“Katika ukaguzi tulioufanya, tumebaini tatizo kubwa kwenye matumizi, watu wamegeuza shule kuwa kichaka cha kutafuna fedha, sasa hawa tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria,” alisema Bulembo.

Alitoa mfano wa walimu wa shule za Tegeta, Tabata na Mwembe Tongwa ambao wameshafikishwa mahakamani kutokana na ubadhirifu. 

Aidha, Bulembo alisema taasisi yake imejizatiti katika kuhakikisha inabaki katika soko la elimu kwa kuimarisha na kutoa elimu bora katika shule wanazomiliki.

“ Kwa sasa Serikali imejipanga kuboresha shule zake, hivyo kutakuwa na ushindani wa kupata wanafunzi, ili tubakie kwenye soko ni lazima tuimarishe shule zetu,” alisema. 

Bulembo alisema pia taasisi yake imejikita katika kuanzisha vyuo mbalimbali vya elimu ya juu kwa fani mbalimbali ikiwamo kozi ya ualimu.

Akizungumzia ada elekezi, Bulembo alisema anaamini serikali itakuja na ada elekezi ambayo inaendana na wakati uliopo kwani kuendesha shule kuna gharama nyingi ambazo mzazi anachangia kupitia ada.

Serikali pamoja na kufuta ada kwa shule inazozimiliki kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne, inakusudia kuja na ada elekezi kwa shule binafsi lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...