Skip to main content

Jecha wa ZEC Atoka Mafichoni.....Dk. Shein Asisitiza Uchaguzi Lazima Urudiwe Zanzibar


Hatimaye  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, jana ameonekana hadharani katika maadhimisho ya
sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Jecha ambaye inaaminika alikuwa mafichoni tangu alipotangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Oktoba 28, mwaka jana, alionekana ameketi kwenye jukwaa kuu la viongozi, jirani na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Kuonekana kwa Jecha hadharani kumezua mijadala mitaani na hata katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakihoji alikuwa wapi mara baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi.

Watu mbalimbali wamekuwa wakihoji kuonekana kwa Jecha hadharani jana, siku ambayo Dk. Shein alitumia maadhimisho ya Mapinduzi kutangaza kwamba uchaguzi wa marudio Zanzibar iwe isiwe utafanyika.

Oktoba 28, mwaka jana majira ya saa sita mchana kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilizopo Kilimani mjini Unguja, ilikuwa ndiyo siku ya mwisho kuonekana Jecha hadharani.

Siku hiyo huku akiwa chini ya ulinzi wa vijana wawili wanaoaminika kuwa ni makomandoo wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania (JWTZ) waliovaa kiraia, Jecha alitangaza kuufuta uchaguzi wa Zanzibar mbele ya vyombo vichache vya habari.

Alitumia dakika mbili tu kuvitangazia vyombo hivyo vya habari juu ya adhima yake ya kuufuta uchaguzi na kutoa sababu zilizomfanya kufanya hivyo ikiwamo kuharibiwa kwa uchaguzi kisiwani Pemba.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kutoa taarifa yake kwa vyombo hivyo, Jecha hakutaka kuulizwa maswali.

Oktoba 27, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi, Jecha pia hakuonekana kwenye kituo cha kutangaza matokeo kilichokuwa katika Hoteli ya Bwawani kwa kile kilichodaiwa alipata matatizo ya kiafya na hivyo kumwachia kazi hiyo Makamu Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Abdulhakim Ameir Issa.

Siku hiyo majira ya saa kumi jioni, askari wa JWTZ walizingira kituo cha Bwawani na kuwaamuru watu waliokuwa ndani kutotoka nje na hata wale walioko nje ya kituo hicho kutosogea.

Watu waliokuwa ndani ya kituo hicho wengi wao walikuwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi pamoja na baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa waliofika kusikiliza matokeo ya uchaguzi.

Dr. Shein asisitiza Uchaguzi lazima urudiwe
Kutokana na kile kinachoonekana kuendelea kupasuka kwa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesisitiza uchaguzi utarudiwa baada ya awali matokeo yake kufutwa na ZEC.

Akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amaan jana, Dk. Shein alisema uchaguzi huo utarudiwa kwa mujibu wa katiba na sheria.

“Kila mmoja anajua kilichotokea katika uchaguzi Zanzibar baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi kutokana na kasoro zilizogundulika kutokea wakati wa uchaguzi huo,”alisema Dk. Shein na kuongeza:

“Suala la kurudiwa kwa uchaguzi liko palepale na utarudiwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo nawaomba wananchi muwe na uvumilivu na upendo wakati tukisubiri kutangazwa kwa tarehe ya kurudiwa uchaguzi.”

Licha ya kwamba kila upande umeshaweka msimamo wake, lakini Dk. Shein alisema mazungumzo ya kusaka suluhu yanaendelea baina ya pande hizo na kwamba taarifa ya mazungumzo hayo itatolewa punde yatakapokamilika.

“Tangu kutokea kwa mgogoro huu tulishauriana kukutana viongozi sita waliopo madarakani na waliostaafu ili kufanya mazungumzo ya kusaka suluhu na taarifa itatolewa pindi mazungumzo yatakapokamilika,”alisema Dk. Shein

Comments

Popular posts from this blog

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HAYA NDO MANENO YA KUMPANDISHA hisia MPENZI WAKO UMPENDAE!!!!!

                                       Inawezekana wengi wetu tukawa tunayatumia bila kujua kwamba tumekusidia kuyatumia. Haya ni maneno au kauli ambazo mume/mke anaweza mwambia mwenza wake kama ishara ya kumpandisha "nyege" kabla ya kuanza  kufanya mapenzi. Wawili hawa wanaweza wakawa sehemu tofauti tofauti, mfano mume yupo kazini lakini anakaribia kurudi nyumbani, mke ukaanza "kumcharura" mumeo kwa kauli mbali mbali aidha kupitia sms au kwa kumpigia simu, ingawa kupitia sms ndo inasisimua zaidi! Hapa najua naongea na watu wazima, sina haja ya kuandika zaidi maneno yenyewe lakini kila mmoja ni mjuzi wa tabia na vitu ambavyo mwenza wake anavihusudu hasa mkiwa kitandani, mfano" Baby ukirudi leo nataka unipindishe pale katika dressing table kama ulivyonifanyia jana, na leo nimevaa lile gauni ulipendalo na zile bikini mpya, dont be late my love" Maneno haya kwa anayejua mapenzi na anampenda mkewe ni lazima huko alipo "Jogoo" awike kidog

HUYU NDIYE ALIIYELAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI NA MBWA PAMOJA NA FARASI KWA AJILI YA PESA.

When the Internet first came to the continent of  African society,most people were  very pleased with it because it reduces stress of communication with love around the world,it also serve as productive purposes like communication.It served many people for chatting, sending mails and even business. As the time passed by many ladies discovered that they could use the internet to find a chat friend or a life partner.Some girls have greatly benefited just by using the internet to find their dream marriages or relationhsips. Others have fallen into traps in the West and wish they would never have known what the internet was.This is the case of one Cameroonian,Elvire Axelle Tchamakoua. Continue....... SEE HOW IT ALL HAPPEN.... Axelle is pr00stit-te who is pimped to various men by her main man Jean Claude(French Businessman).She did not mind serving her customers from the front or from behind.The use of condoms during her encouters was the allowed as it b