Skip to main content

"Mimi ndiye Rais Halali wa Zanzibar na Nisiposema Mimi Nitawatuma Wasaidizi wangu Kuwaeleza" - Dk Shein


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kutoa changamoto kwa wasioiamini Katiba hiyo kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo ndiyo pekee yenye uwezo wa kutafsiri Katiba.

Amebainisha kuwa yeye anaongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwamba kama si uwezo huo aliopewa Kikatiba hana sababu ya kuendelea kukaa madarakani pamoja na serikali anayoingoza.

“Tuko madarakani na uongozi wote wa serikali… yupo Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rais na mawaziri” alisisitiza Dk. Shein na kuongeza kuwa hao wanaodai kujiondoa serikalini huo ni uamuzi wao wenyewe.

Alibainisha kuwa yeye na serikali anayoingoza kuendelea kuwepo madarakani “si uamuzi wake” na wala yeye hana “ubavu” wa kujiweka madarakani bali ni Katiba ambayo inajieleza wazi.

Dk. Shein ametoa kauli hiyo jana kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu kisiwani humu kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi.

Aliwaambia wananchi hao kuwa yako mengi yanayosemwa lakini hawapaswi kuyasikiliza kwa kuwa kama ni serikali yeye ndiye Rais hivyo wanapaswa kumuamini anachowaeleza.

“Ya mjini yapo yasikilizeni lakini kwa Serikali mimi ndiye Rais na nisiposema mimi nitawatuma wasaidizi wangu kuwaeleza” Dk. Shein alibaisha na kuongeza kuwa ya vyama kila mtu ana chama chake.

Alifafanua kuwa kama ni suala la Chama cha Mapinduzi (CCM) yeye ndiye Makamu Mwenyekiti Zanzibar na kama kuna la kuwaeleza wana CCM na wananchi atawaeleza yeye na viongozi wenzake wa chama hicho pamoja na taarifa za vikao vya chama vyake.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa ushindani wa kisiasa si ugomvi bali ni utaratibu wa kupeana changamoto katika uongozi ambao lengo ni kuwaletea wananchi maendeleo.
  
“tusikejeli maendeleo yetu, tuthamini chetu na ushindani wetu wa kisiasa usirejeshe nyuma maendeleo yetu” Dk. Shein alitahadharisha.

Dk. Shein aliruejea wito wake wa kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yameanza tarehe 3 Januari na yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 12 Januari, 2016 katika kiwanja cha Amaan.

Aliwakumbusha wananchi hao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yaliyomfanya Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume kutangaza Jamhuri ya Zanzibar, ndiyo yaliyowakomboa wanyonge wa Visiwa vya Zanzibar kwa kuondosha aina zote za ubaguzi na kuwapa mamlaka ya kujiamulia mambo yao.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi wa Pemba kuwa meli mpya iliyonunuliwa na Serikali MV Mapinduzi II ambayo ilizinduliwa hivi karibuni, itawasili kisiwani humo tarehe 10 Janauri na siku itakayofuata itawachukua baadhi ya wananchi kwenda Unguja kushiriki maaadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi.

Alisisitiza kuwa serikali itawalipia gharama za usafiri wa kwenda na kurudi Unguja wale wote watakaoteuliwa kuwemo kwenye safari hiyo kufuatana na utaratibu utakaowekwa kama alivyokuwa ameahidi wakati meli hiyo ilipokuwa inatengenezwa nchini Korea ya Kusini.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais amefuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wabunge

Comments

Popular posts from this blog

ANGALIA VIDEO YA MWANAMKE AKIZINI NA CHUPA YA SODA YANASWA

 Katika  hali  ya  kushangaza  na  kuashiria  miisho  ya  dunia, binti  mmoja  amenaswa  " live " akifanya  mapenzi  na  CHUPA YA SODA. Katika  video  hiyo, binti  huyo  anaonekana  akitoa  ushirikiano  wa  kutosha  mithili  ya .............

HUYU NDIYE ALIIYELAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI NA MBWA PAMOJA NA FARASI KWA AJILI YA PESA.

When the Internet first came to the continent of  African society,most people were  very pleased with it because it reduces stress of communication with love around the world,it also serve as productive purposes like communication.It served many people for chatting, sending mails and even business. As the time passed by many ladies discovered that they could use the internet to find a chat friend or a life partner.Some girls have greatly benefited just by using the internet to find their dream marriages or relationhsips. Others have fallen into traps in the West and wish they would never have known what the internet was.This is the case of one Cameroonian,Elvire Axelle Tchamakoua. Continue....... SEE HOW IT ALL HAPPEN.... Axelle is pr00stit-te who is pimped to various men by her main man Jean Claude(French Businessman).She did not mind serving her customers from the front or from behind.The use of condoms during her encouters was the allowed as it b

HAYA NDO MANENO YA KUMPANDISHA hisia MPENZI WAKO UMPENDAE!!!!!

                                       Inawezekana wengi wetu tukawa tunayatumia bila kujua kwamba tumekusidia kuyatumia. Haya ni maneno au kauli ambazo mume/mke anaweza mwambia mwenza wake kama ishara ya kumpandisha "nyege" kabla ya kuanza  kufanya mapenzi. Wawili hawa wanaweza wakawa sehemu tofauti tofauti, mfano mume yupo kazini lakini anakaribia kurudi nyumbani, mke ukaanza "kumcharura" mumeo kwa kauli mbali mbali aidha kupitia sms au kwa kumpigia simu, ingawa kupitia sms ndo inasisimua zaidi! Hapa najua naongea na watu wazima, sina haja ya kuandika zaidi maneno yenyewe lakini kila mmoja ni mjuzi wa tabia na vitu ambavyo mwenza wake anavihusudu hasa mkiwa kitandani, mfano" Baby ukirudi leo nataka unipindishe pale katika dressing table kama ulivyonifanyia jana, na leo nimevaa lile gauni ulipendalo na zile bikini mpya, dont be late my love" Maneno haya kwa anayejua mapenzi na anampenda mkewe ni lazima huko alipo "Jogoo" awike kidog