Skip to main content

Serikali Kugawa BURE Mbegu za Mazao Yanayohimili Ukame kwa Wananchi Wanao kabiliwa na Njaa


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imeanza mkakati wa menejimenti ya maafa ya ukame kwa kuwawezesha wananchi wanao kabiliwa na njaa kuweza kukabili maafa hayo kwa kuwagawia wananchi hao mbegu bure za mazao yanayohimili ukame katika halmashauri husika.

Kufuatia hali ya ukame ambao umezikumba baadhi ya halimashauri hapa nchini katika msimu wa 2014/2015, baadhi ya halmashauri hizo zilipata upungufu wa chakula hali iliyopelekea halmashauri hizo kuomba chakula cha msaada Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu maafa.

Akiongea wakati wa ziara ya kukagua hali ya upungufu wa chakula katika kata ya Malengamakali, wilayani Iringa Tarehe 11 Januari, 2016, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa mkakati uliopo ni kuwahamasisha wananchi walime mazao yanayohimili ukame.

“Nashauri watendaji wakuu wa Halmashauri na mikoa kupitia kamati za maafa waorodheshe wananchi wote wanaohitaji mbegu hizo na kuwasilisha katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa na Ofisi yangu itatuma fedha za kununua mbegu hizo ili zigawiwe bure kwa wananchi wengine wenye upungufu wa chakula, tunahitaji wananchi wote wawe na uhakika wa chakula .” amesema Brig. Jen. Msuya.

Awali akiongea katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Iringa, Richard Kasesela, alibainisha kuwa katika kukabiliana na upungufu wa hali ya chakula halmashauri hiyo imefanya uhamasishaji wa kilimo cha zao la Mtama amabalo ni zao linalovumilia ukame na mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi kama vile viazi vitamu.

“Uhamasishaji umefanyika katika Tarafa za Isimani, Idodi, Pawaga na Kalenga (mfyome), tumeanzisha na sheria ndogo ya kilimo ambayo inaitaka kila kaya kulima mtama ekari mbili katika kata hizi na atakayekiuka sheria hii adhabu yake ni kulipa kiasi cha fedha shilingi 50,000/=” alisisitiza Kasesela.

Katika kukabiliana na upungufu wa chakula Halmashauri ya Iringa iliomba chakula cha msaada kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa, ikiwa hadi kufikia Disemba 2015, tayari tani 4, 546 zilikuwa zimeletwa wiliyani humo ambazo zimesambazwa katika Kata 11, vijiji 42 katika maeneo yenye upungufu wa chakula.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...