Skip to main content

Wizara ya Afya yatoa Taarifa ya Ugonjwa wa Kipindupindu Nchini.


 Na Skolastika Tweneshe-Maelezo
Jiji la Dar es salaam limeripotiwa kutokuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu  kuanzia Desemba mwaka jana.

Akizungumza leo na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam  Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mh. Dkt Hamisi  Kigwangalla amesema kuwa licha ya ugonjwa wa kipindupindu kuanzia jijini Dar es salaam na kudumu kwa miezi minne lakini kwa sasa hajaripotiwa mgonjwa wa kipindupindu.

“Mkoa wa Dar es salaam ambako ndipo ugonjwa ulipoanzia na kudumu kwa miezi minne haujaripotiwa  kuwa mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015,” alisema Kigwangalla.

Waziri Kigwangalla aliongeza kuwa mikoa mingine ambayo haijaripotiwa kuwa na maambukizi kwa muda wa wiki moja ni pamoja na Mbeya,Rukwa,Katavi,Kigoma,Kagera  na Lindi.

Aidha  alisema kuwa mikoa ambayo haijarioptiwa ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni  Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa  pia amesema kuwa kuna mikoa ambayo haijawahi kuripoti tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze nayo ni mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Dkt. Kigwangalla alitaja mikoa iliyotoa idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu ambayo ni Halmashauri ya Morogoro(66), Arusha (50), Singida(40), na manispaa ya Dodoma (33).

Pia amewaasa wananchi  kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama pamoja na kunawa mikono na maji safi na sabuni kwa maji safi yanayotiririka pamoja na kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji ,maziwa na mabwawa.

Kwa mujibu wa wizara ya afya tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua kipindupindu, na kati yao watu 205 wameshafariki kutokana na  ugonjwa huo

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...